KUPANDA KWA MAFUTA NI DUNIA NZIMA WANANCHI WAJIHADHARI NA WAPOTOSHAJI
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kenan Kihongosi, amezungumza na wanahabari leo jijini Dodoma na kuwahakikishia wananchi kwamba Serikali imeanzisha mfuko maalum kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa mafuta. Aidha Chama cha Mapinduzi kimeitaka Serikali kuhakikisha inalitumia shirika la TPDC kuwa muagizaji mafuta mkuu ili kuwauzia wananchi kwa bei ya soko kwani baadhi ya wafanyabishara huwa na mambo yao kwa kujali faida zaidi. Kihongosi amebainisha kwamba hakuna nchi ambayo haijaguswa na kupanda kwa mafuta hata kule ulaya mafuta yamepanda kuliko Tanzania hata majirani wa Tanzania mfano hapo Kenya na Uganda bei ipo juu sana kuliko hapa nchini "Mafuta yamepanda kwenye soko la Dunia kutokana na vita vya mashariki ya kati kati ya Marekani, Israel na Irani tuombee vita viishe ili hali ilejee kama kawaida", alisema Kihongosi.
Aidha mewataka wanasiasa kuaacha kutumia uhaba wa mafuta kujitafutia umaarufu
Comments
Post a Comment