VITUO 14 ZA KUJAZIA GESI VYA JIJINI DAR ES SALAAM ----- MKURUGENZI TPDC MAKAME
Aidha amesema mpaka sasa wameweza kuunganisha nyumba 2500 kwa wananchi wa Mtwara kwa ajili ya huduma ya gesi wanataka kushirikiana na watu binafsi kwa ajili hya kusambaza gesi hiyo kuwafikia wananchi mikoani. Makame amebainisha kwamba shieika lake limeweza kufungua vituo 14 vya kujazia gesi jijini Dar es salaam na wapo mbioni kusambaza mikoani sasa.
Makame amesema utekelezaji wa mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki ( EACOP), umefikia asilimia 43.5 huku baadhi ya kazi za ujenzi katika makambi na vituo vya kuhifadhia mabomba zikikamilika kwa asilimia 100.
Pia Wanatalajia kujenga bomba jipya kutoka Mtwara hadi Chalinze ,Tanga na hadi mikoa ya kati, wamo katika upembezi yakinifu maeneo ya Mkuza upembezu huo utachuku mwaka mmoja na nusu kwa mwaka wa fedha huu.
Miradi hiyo inatekelezwa na vijana ambao wanaajiliwa, ajila hiyo ipo ya aiba mbili ya moja kwa moja na ile ya ajira ya muda hiyo yote ni vijana wa nchi hii
Comments
Post a Comment