NAIBU WAZIRI WA KILIMO SILINDE AZINDUA MIRADI SAGCOT, AGRA JIJINI DODOMA

Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde amezindua Miradi itakayosaidia kuleta zaidi mageuzi katika Sekta ya Kilimo, inayofahamika kama SAGCOT: Support to SAGGOT Centre Ltd; na AGRA: Support to Tanzania’s Agriculture Transformation Office.

Dhumuni la miradi hiyo ni kupanua wigo wa maeneo ya Kilimo Tanzania, yaani “The Agriculture Growth Corridors of Tanzania (AGCOT) kufuatia kusainiwa kwa mkataba wa makubaliano kati ya Norway na AGRA.  Makubaliano hayo yamelenga kufungua vikwazo vya udhibiti wa kilimo ikiwa ni pamoja na vikwazo vya mauzo ya nje ili kuvutia uwekezaji wa Sekta Binafsi katika Sekta ya Kilimo nchini kupitia Ofisi ya Mageuzi ya Kilimo (Agricultural Transformation Office - ATO).

Uzinduzi huo umefanyika tarehe 04 Februari 2025 jijini Dodoma na kuhudhuriwa pia na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Tine Tonnes; Mtendaji Mkuu wa Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT), Bw. Geoffrey Kirenga; Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ofisi ya Mageuzi ya Kilimo (Agricultural Transformation Office- ATO), Bw. Jeremiah Temu; Mkurugenzi Mtendaji wa Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA) Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, Prof. Jean Jacques Muhinda pamoja na Wadau mbalimbali wa Sekta ya Kilimo na Mazingira.

Miradi yote itatekelezwa kwa miaka 3 (2025-2027) na itagharimu Dola za Marekani 1,348,466 sawa na shilingi 3,429,186,305 za Tanzania.







Balozi wa Norway nchini Tanzania, Tine Tonnes na Mkurugenzi Mtendaji wa Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA) Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, Profesa. Jean Jacques Muhinda (kulia), wakitia saini 

Wakibadilishana hati baada ya kusaini
Naibu Waziri Silinde akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi

Wakikata keki

Mkurugenzi Mtendaji wa Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA) Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, Prof. Jean Jacques Muhinda



 Wakipiga picha ya pamoja

Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA