VIONGOZI WA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA CHAKUHAWATA WAKUTANA JIJINI DODOMA

VIONGOZI  wa Chama Cha Kulinda na Kutetea Haki za Walimu (CHAKUHAWATA) zaidi ya 400 wamekutana leo jijini Dodoma kwa ajili ya kufanyia marekebisho katiba ya chama hicho, ili iendane na wakati, wameshilikisha wajumbe wote kutoka mikoa ya Tanzania bara. Aidha  Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho Emannuel Patrick, amemuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, aingilie swala la walimu ambao ni wanachama wa chama chao kupewa vitisho na wakurugenzi na makatibu Tawala, alitolea mfano Wilaya nya Mkinga viongozi wao hawatakiwa kufanya vikao, hata mkao wa Mara wamekuwa wakizuiwa pia, baadhi ya viongozi Serikalini wanakipakazia kwamba eti kinajihusisha na vyama vya Siasa. ameomba  waajili waache kuwapaka matope, aidha Tanga  na Singida , Mwanza Kigoma, Tabora na Kariua wananyanyaswa kwa kuzuiwa makato ya wanachama wao. Mwenyekiti huyo amebainisha kunachama kinawapiga vita kutokana na wanachama  wao wengi kuhamia katika chama hicho hivi sasa kina wanachama zaidi ya 4000 nchi nzima

Wengi wa wanachama wanaojiunga na chama hicho wanasema wamekimbia makato ya asilimia mbili huko wanakotoka wanakimbilia Chakiwahata kwani huko kunamakato ya sh 5000 tu kwa mwezi . pia wanalipiwa bima ya Afya wao na familia zao tofauti na watokako kulikojaa mizengwe bila kutolea ufafanuzi ni wapi huko kulikojaa mizengwe na ubadhilifu wa michango yao walimu.

Mmoja wa wanashreria akisimamia marekebisho ya katiba katika mkutano huo

Wanachama wakishiliki kuisuka katiba yao











 

Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA