WALIMU WAHITIMISHA MKUTANO WAO WA SIKU MBILI JIJINI DODOMA
Baadhi ya Viongozi hao ambao ni Wenyeviti na Makatibu wakizungumza na wanahabari baada ya mkutano huo kufungwa waliwashukuru viongozi wao Mwenyekiti ,Katibu Mkuu, Mwekahazina wa Chama chao na kamati tendaji yao kwa kufanikisha mkutano huo, walidai wamepitia katika manyanyaso makubwa kutokana na katiba yao kunyanyapaliwa aidha kucheleweshwa wanachama wao ambao wanamiminika kwa wingi kuingia katika chama chao lakini wanakwamishwa na baadhi ya watendaji serikalini hususan baadhi ya wakurugenzi katika halmashauri nchini. wamemmiminia sifa nyingi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwesha kufanikisha chama hicho kuwepo hadi sasa n akupelekea kuangusha sebene ukumbini kwa kumsifia wakimuombea mitano tena wapo nyumba yake kumuunga mkono hadi kieleweke, Walibainisha kwamba kujiunga na vyama hivi ni hiari lakini wanalazimishwa kubaki katika vyama ambavyo hawaoni manufaa yao vyama wanakokimbia vimejaa migogoro na ufujaji wa fedha za wanachama . Mwenkahazina wa chama hicho akizungumza na wanahabari alisema Mkutano huo wa siku mbili wametumia fedha zao za makato ya sh elfu 5 hawakuwa na wafadhili kama vyama vingine vinavyofanya pamoja na kupatiwa mamilioni ya fedha za makato ya walimu kutoka Serikalini. "Njoni chakuhawata makato ni buku tano tu na siyo asilimia mbili na kunafaida nyingi achaneni na vyama vya utafunaji fedha za michango yenu" alisema Mhazini huyo bila kutaja vyama hivyo..
Mwenyekiti Emmanuel na Katibu Mkuu wa Chama hicho Twalib Nyamkungu wakibadilishana mawazo baada ya kufungwa mkutano huo
Wakiwaaga viongozi wao
Wakisakata muziki huku wakimshukuru rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa upendo wake na kumuombea mitano tena
Comments
Post a Comment