SEKTA YA NISHATI MANENO KIDOGO VITENDO ZAIDI - DKT. BITEKO
📌 Ashiriki Bonanza la Nishati Dodoma 📌 Ataka Watumishi kupendana na kushirikiana 📌 Atunukiwa Nishani ya Uasisi Bonanza la Nishati 📌 EWURA yaibuka mshindi wa Jumla; Mkurugenzi Mkuu amshukuru Dkt.Biteko kuthamini Watumishi Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe, Dkt. Doto Biteko amewakumbusha Watumishi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake kuiishi Kauli Mbiu ya Sekta ya Nishati ambayo ni Maneno Kidogo Vitendo zaidi ili kuweza kutoa huduma iliyobora kwa wananchi. Amesema hayo leo tarehe 27 Julai 2024, wakati Watumishi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake waliposhiriki kwenye Bonanza la Nishati ambalo limefanyika Jijini Dodoma likibebwa na Kaulimbiu Shiriki Michezo Imarisha Afya. “Sekta ya Nishati ni muhimu kwenye ujenzi wa uchumi wa nchi yetu na tufahamu kwamba Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatutegemea sisi ili kuweza kutoa huduma hii muhimu kwa wananchi, hivyo watumishi tupendane, tushirikiane na kufanya kazi kwa bidi zaidi ili kusukuma mbele gurudumu la N