Posts

Showing posts from February, 2024

YANGA SC YATINGA ROBO FAINALI CAFCL,YAICHAPA 4G CR BELOUIZDAD

Image
TIMU ya Yanga SC imeandika historia ya kufuzu hatua ya robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya  CR Belouizdad ya Algeria mchezo wa hatua ya Makundi uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Mabao ya Yanga SC yamefungwa na Mudathir Yahya dakika ya 43,Stephane Aziz Ki dakika ya 46,Kennedy Musonda dakika ya 48 na Joseph Guede dakika ya 84. Kwa ushindi huo Yanga wamefikisha Pointi 8 huku Al Ahly wakiwa na Pointi 9 ,nafasi ya tatu CR Belouizdad Pointi 5,Medeama Pointi 4 mchezo wa mwisho Yanga itasafirisha kwenda Misri kucheza na Al Ahly. Yanga SC imefuzu moja kwa moja kwa kuwa Mbabe wa ‘head to head’ kati yake na CR Belouizdad kwa maana hata kama CR Belouizdad atashinda mechi yake ya mwisho hawezi kufuzu. Itakumbukwa mechi ya kwanza Yanga ilifungwa mabao 3-0 kabla ya leo kushinda mabao 4-0 kwenye mchezo wa marudiano.

INDIA YATANGAZA NEEMA KWA ZAO LA MBAAZI NCHINI

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akisalimiana na Waziri wa Biashara na Viwanda wa India Mhe. Piyush Goyal walipokutana kwa mazungumzo ofisini kwake jijini New Delhi. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akifurahia jambo na Waziri wa Biashara na Viwanda wa India Mhe. Piyush Goyal walipokutana kwa mazungumzo jijini New Delhi.  Mazungumzo yakiendeleaa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akiwa na Waziri wa Biashara na Viwanda wa India Mhe. Piyush Goyal baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ofisini kwake jijini New Delhi. @@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@ Tanzania imeruhusiwa kuiuzia India kiasi cha mbaazi inachoweza kuanzia sasa hadi Machi 2025. Makubaliano hayo yamefikiwa leo tarehe 24 Februari 2024 wakati wa mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba, na Mwenyeji wake Waziri wa Biashara

WAKASUVI AMEFIKWA MAUTI KATIKATI YA JUKUMU ZITO: DKT. NCHIMBI.

Image
  SHARE Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi amesema kuwa kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Ndugu Hassan Mohamed Wakasuvi ni pigo kubwa, si kwa mkoa huo pekee, bali Chama, Serikali na taifa zima kwa ujumla, ambapo amefikwa na mauti akiwa ni Mwenyekiti wa Kamati Ndogo, iliyopewa jukumu la kuangalia namna ya kukiboresha Chama Cha Mapinduzi.     Dk. Nchimbi amesema kuwa Komredi Wakasuvi alikuwa mmoja wa viongozi shupavu wa Chama Cha Mapinduzi, kuanzia mkoani kwake, hadi ngazi ya taifa, ambapo kutokana na uwezo na uadilifu wake katika kutimiza majukumu yake kwa ufanisi na ushirikiano tangu alipochanguliwa kuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa CCM, mwaka 2007, aliendelea kuaminiwa hadi kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, nafasi aliyokuwa nayo hadi mauti yalipomfika.     Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Nchimbi amesema hayo alipokuwa akitoa salaam za pole na rambirambi kwenye msiba wa Mzee Wakasuvi, kabla ya mazis

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA HUDUMA BORA MLOGANZILA

Image
Na.WAF, Dar Es Salaam Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Maswala ya UKIMWI imeridhishwa na hali ya utoaji huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kuanzia kwa wafanyakazi, vifaa bora na vya kisasa vya kutolea huduma ambapo pia mazingira yanaridhisha na wagonjwa wanahudumiwa vizuri. Hayo yamebainishwa leo na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, Dkt. Faustine Ndugulile baada ya ziara ya kamati ya kutembelea hospitali hiyo na kukagua maboresho ya miundombinu iliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. Dkt. Ndugulile amesema Serikali imefanya uwekezaji mkubwa wa kujenga hospitali hiyo ambapo pia kuna kituo kingine cha utafiti wa magonjwa ya moyo ambacho kimejengwa katika eneo hilo. “Niipongeze Serikali kwa kuboresha huduma za afya nchini kwani hivi sasa asilimia 90 ya wagonjwa ambao walikuwa wanakwenda nje ya nchi kutibiwa wanatibiwa hapa nchini na tumeanza ku

RAIS SAMIA ATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA ALIYEKUWA RAIS WA NAMIBIA HAYATI DKT. HAGE GEINGOB

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Namibia Marehemu Dkt. Hage Geingob katika uwanja wa Michezo wa Uhuru Jijini Windhoek tarehe 24 Februari, 2024. Hayati Rais Geingob alifariki dunia tarehe 04 Februari na anatarajiwa kuzikwa tarehe 25 Februari, 2024 katika Makaburi ya Mashujaa ya Heroes’ Acre Jijini Windhoek Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia katika mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Namibia Marehemu Dkt. Hage Geingob kwenye uwanja wa Michezo wa Uhuru Jijini Windhoek tarehe 24 Februari, 2024. Hayati Rais Geingob alifariki dunia tarehe 04 Februari na anatarajiwa kuzikwa tarehe 25 Februari, 2024 katika Makaburi ya Mashujaa ya Heroes’ Acre Jijini Windhoek Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimfariji Mjane wa Marehemu Monica GeingoGeingob mara baada ya kuzungumza na kutoa heshim

VIONGOZI WA JUMUIYA YA MARIDHIANO MKOA WA DODOMA YAHAMASISHA KUFANYA USAFI

Image
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), mkoa wa Dodoma, Profesa. Emmanuel Shija, akihutubia wakazi wa mtaa wa Chinangali Baada ya kumaliza kufanya usafi  katika makaburi yaliyopo kando kando mwa shule ya Chinangali, usafi huo uliambatana na utoaji wa damu katika Zahanati ya Chamwino  .Wengine ni viongozi wa wilaya na mkoa huo. Mtendaji wa mtaa huo akihutubia wananchi Wakazi hao wakifanya usafi Mkuu wa idara ya Mazingira Wilaya ya dodoma, akizungumza Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Wilaya ya Dodoma, akizungumza Katibu wa Jumuiya ya Maridhiano Mkoa wa Dodoma ,akizungumza Zahanati ya Chamwino ambapo alifika na kutoa damu kwa wahitaji Wananchi hao wakitoa damu Mganga wa zamu wa Zahanati hiyo Perpetua Kasase, akizungumza na viongozi waliofika katika zahanati hiyo