NAIBU WAZIRI KAPINGA AWASHA MIRADI YA UMEME YA 20-BILIONI MOROGORO KUSINI
Na.Issa Sabuni na Zuwena Msuya, Morogoro Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amewasha umeme kwa mara ya kwanza katika vijiji viwili vya jimbo la Morogoro Kusini na kuwahamasisha wananchi kusuka umeme (Wiring) kwenye nyumba zao ili kuutumia katika kuleta maendeleo. Naibu Waziri amesema hayo leo, Novemba 30, 2023 wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya umeme vijini na kuwasha Umeme Tayari (UMETA) katika Kata ya Mvuha wilaya ya Morogoro Vijijini. Naibu Waziri Kapinga amewahamasisha wananchi hao kuunganisha umeme kwani serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi katika miradi lengo likiwa ni kuwainua kiuchumi. Amewapongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kutekeleza miradi ya umeme vijijini na kuwaahidi wananchi kuwa serikali itahakikisha kuwa vijiji vyote vinafikiwa ifikapo Juni 30, 2024. Aidha amewashauri Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme nchini, TANESCO kuja na mpango mkakati utakaowawezesha wananchi wengi kusuka waya kwenye nyumba (wirin