SIDO MBEYA WAMWELEZA MATATIZO YAO NAIBU WAZIRI KIGAHE BAADA YA KUWATEMNELEA

Naibu Wazoro Kigahe, akionyeshwa eneo la Sido Mbeya lilivyo kubwa
Naibu Wazori Kigahe, akizungumza na maofisa wa SIDO Mbeya kabla ya kuanza kukaguwa

Baadhi ya mashine za kuchongea vyuma zikiwa katika jengo la SIDO mbeya

 Naibu Waziri akikagua mashine zilizofungwa tayari kwa kufanya kazi jijini Mbeya

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UWEKEZAJI, VIWANDA NA
BIASHARA
SHIRIKA LA KUHUDUMIA VIWANDA VIDOGO
TAARIFA YA SHUGHULI ZA SIDO MKOA WA MBEYA KWA MWAKA
WA FEDHA 2016/2023 KWA MUHESHIMIWA EXAUD SILAONEKA
KIGAHE (MB.) NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA
TAREHE 06/08/2023
1.0 Kwa niaba ya uongozi wa shirika,napenda kuchukua fursa hii
kukushukuru sana wewe binafsi, kwa kuja kutembelea mkoa wa
Mbeya na maalum kwa kuwa na ratiba ya kutembelea SIDO Mbeya ili
kupata taarifa na kujionea baadhi ya shughuli ambazo tunafanya katika
kuchochea uanzishwaji na uendelezaji wa viwanda vidogo na biashara
ndogo na hatimaye utupe maelekezo na ushauri utakaotupa msukumo
katika jitihada zetu za ujenzi wa uchumi wa viwanda ili kutengeneza
fursa za ajira, kipato cha mtu mmoja mmoja na pato la taifa .
Mheshimiwa Naibu Waziri;
2.0 SIDO tangu kuanzishwa kwake mwaka 1973 inayo majukumu
ya kutoa huduma ambazo zinawawezesha kuchochea uanzishwaji na
uendelezaji wa viwanda vidogo nchini Tanzania. Hivyo muda wote
SIDO imekua na majukumu ya kutoa huduma ambazo zinawezesha
Jasiriamali ndogo na za kati kujijengea uwezo wa kuanzisha na
kuendeleza viwanda vidogo, na hususani vinavyolenga uongezaji wa
mnyororo wa thamani ya mzao asilia na yanayozalishwa katika mikoa
miwili ambayo tunaisimamia na hasa kutoka vijijini.
Mheshimiwa Naibu Waziri;
3.0 Kwa kuzingatia umuhimu wa sekta ya viwanda vidogo na vya
kati kwenye uchumi wa taifa na uzoefu tulioupata ndani na nje ya nchi
, sekta hii ina umuhimu mkubwa na wapekee katika kuongeza thamani
ya mazao , kuongeza au kutengeneza fursa za ajira kwa wingi ,
kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na pato la taifa kwa ujumla.
Kwa kuzingatia umuhimu huo SIDO Mbeya tumeendelea kutoa
huduma zinazopelekea kuchochea uanzishwaji na uendelezaji wa
viwanda kwenye mikoa tunayosimamia ya Mbeya na Songwe kwa
kutumia mbinu mbalimbali ili kutimiza matakwa ya sheria Na. 8/1973
iliyoanzisha SIDO. Miongoni mwa mbinu hizo ni kutoa mafunzo
mbalimbali , huduma za teknolojia na ufundi, mitaji ya uwekezaji na
geugeu, miundombinu hasa majengo kwa ajili ya uzalishaji , ukuzaji
wa masoko ya bidhaa wanazozalisha na kutoa mbinu mbalimbali za
uanzishaji viwanda kwa mfumo wa makongano ( industrial clusters).
Katika kutekeleza shughuli za shirika kwa mwaka wa fedha 2022/2023
tunaishukuru serikali kwa kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara kwa
kutupataia fedha Tsh 200,000,000/= kwa ajili ya ujenzi wa
miundombinu katika soko la SIDO Mwanjelwa pamoja na mashine
mpya 6 na komputa mpakato moja kwa ajili ya kituo cha uendelezaji
wa teknolojia.
Fedha za ujenzi wa miundombinu zilitegwa kwa ajili ya ujenzi wa
mitaro na kalvat, lakini tumeweza kusimamia kiasi cha fedha
kilichoidhinishwa na kufanikiwa kujenga mitaro ya maji katika soko lote
la Mwanjelwa , ujenzi wa kalvati pamoja na barabara kwa kiwango cha
changarawe.Kwa sasa katika soko hilo hakutakuwa na kero ya
kufurika maji ya mvua kutokana na mifereji iliyojengwa kuweza
kukusanya maji yote na kuyaelekeza katika mtaro mkuu wa tarula.
Mheshimiwa Naibu Waziri;
4.0 Ili kutimiza azma ya Serikali kuifanya Tanzania kuwa na uchumi
unaotegemea viwanda zaidi ifikapo 2025 shughuli ya kuchochea
uanzishwaji na uendelezaji wa viwanda SIDO Mbeya tumeendelea
kupata usaidizi kutoka serikalini kugharimia shughuli mbalimbali na
kutoka kwa wadau zikiwemo taasisi za serikali na binafsi kama ; TBS,
TEA/SDF, TIC, GS 1 (TZ) LTD, CARITAS NA MAENDELEO, HEIFER
INTERNATIONAL, USAID/DAI FEED THE FUTURE ADVANCING
YOUTH SHOP nakadhalika. Ushirikiano huu umewezesha kutimiza
baadhi ya majukumu yetu ya kuchochea kuanzishwa na kuendeleza
viwanda vidogo na vya kati ili kutimiza matakwa ya kisheria
yaliyoanzisha SIDO.
Mheshimiwa Naibu Waziri;
5.0 Takwimu za huduma zilizotolewa kwa kipindi cha miaka nane
2016 hadi 2023 na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO-Mkoa
wa Mbeya kwa Mikoa ya Mbeya na Songwe ambayo tunasimamia ni
kama ifuatavyo:-
I. SHUGHULI ZA KITUO CHA UENDELEZAJI TEKNOLOJIA
Kwa kipindi cha 2016 hadi 2023 kituo kiliendelea kutoa ushauri kwa
wajasiriamali, kutengeneza mashine, vipuri na kukarabati mitambo ili
kuchochea uanzishwaji na uendelezaji viwanda vidogo mijini na vijijini.
Katika kipindi hicho kituo kilitengeneza jumla ya mashine 693 na kama
matokeo kutengeneza ajira 2,772, pia kituo kilifanikiwa kutengeneza
mashine 558 kwa ajili ya kunawia mikono wakati wa janga la korona.
Aidha katika kipindi hicho kituo chetu kilifanya ukarabati wa mitambo
kwenye viwanda vya; Mufindi Tea CO, Kibena Tea CO, Luponde Tea CO,
Ikanga Tea CO, Coca Cola , TBL, Shanta Gold Mining, Wakulima Tea
CO, Total Gases Chico,Tanwat Njombe na TAZARA. Pia kituo kiliweza
kuongeza ubunifu katika mashine tatu ambazo ni mashine ya kuchenjua
dhahabu (Chunya) ambayo imekuwa ikiongeza uzalishaji kwa kuzuia
upotevu wa dhahabu na mashine nyingine ni yakusaga mawe ili kupata
unga kwa ajili ya kukamatisha dhahabu pamoja na mashine ya kupepeta
mazao kama mahindi, ulezi, maharange kwa kuiongezea uwezo kutoka
tani 1 kwa saa hadi tani 3 kwa saa .
MTAWANYO WA UTENDAJI KWA MWAKA NI KAMA IFUATAVYO:
NA MWAKA ODOP NON ODOP IDADI YA
MASHINE
1 2016 43 40 83
2 2017 44 124 168
3 2018 42 80 122
4 2019 54 26 80
5 2020 20 44 64
6 2021 29 38 67
7 2022 38 40 78
8 2023 34 48 82
JUMLA 304 389 693
MHESHIBIWA NAIBU WAZIRI.
Tunashukuru kwa serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara kutupatia
Mashine kwa ajili ya Kituo chetu cha Uendelezaji wa Teknolojia. Mashine
hizo tulizopokea ni kama zifuatazo:- Universal Milling Machine,Hydrolick
Guillotine Shear Machine,Power Diven Metal Plate Rolling,CNC Hydrolick
Press Breke Banding Machine, Automatic (CNC) Plasma Cutting, Synergic
MIG/TIG Welding Machine na Laptop moja zenye thamani ya Dolla za
kimarekani 155,000/= sawa na Fedha za Kitanzania Tshs.370,000,000/=
UFUNGAJI WA MASHINE HIZO (INSTALLATION)
Tayari tulishafanya mawasiliano kupitia Makao Makuu, Mgavi wa Mashine
hizo ameshatuma mafundi leo 06/08/2023 kuja kufunga mashine hizo. Aidha
ufungaji wa mashine hizo utaanza kesho tarehe 07/08/2023 na kuanza
kutumika mara moja baada ya kumalizika kufungwa.
II. SHUGHULI YA UHAMASISHAJI WA UANZISHWAJI VIWANDA
Shughuli ya uhamasishaji uanzishwaji wa viwanda iliendelea katika
kipindi hicho kwa kutoa ushauri wa teknolojia, mpangilio wa mashine
katika viwanda, ushauri kuhusu udhibiti ubora kwa kushirikiana na TBS
na kuwapatia wanaviwanda wapya maeneo ya kufanyia kazi yenye
miundombinu katika maeneo ya mitaa ya viwanda yanayomilikiwa na
SIDO. Jumla ya viwanda 1176 vilianzishwa kufuatia huduma hizo
katika kipindi cha 2016 hadi 2023, viwanda vilianzishwa katika
maeneo ya utengenezaji wa sabuni madawa na mafuta ya kujipaka,
usindikaji wa vyakula mbogamboga na matunda, uchakataji wa
mpunga, kuzalisha unga na kufungasha, vinywaji laini na vikali,
viwanda vya kuchakata maziwa na batiki, tie and die.
Aidha uhamasishaji wa uanzishwaji wa viwanda kwa mfumo wa
kongano (Industrial Clusters) ulifanyika katika ngazi ya mkoa na
kwenye Halmashuri za wilaya mbalimbali.
III. MAFUNZO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI
Ili kuwajengea uwezo wajasiriamali kuona fursa na kuanzisha viwanda
na Miradi midogo SIDO Mbeya imeendelea kutoa mafunzo katika
maeneo ya makazi ya usindikaji wa vyakula mbogamboga namatunda,
batiki, tie and die, utengenzeaji wa Sabuni, mafuta, vipodozi na dawa
za usafi, ujasiriamali na usimamizi wa biashara , kuweka na kukopa na
uundaji wa vikundi. Katika kipindi cha 2016 hadi 2023 jumla ya
mafunzo yaliyotolewa yalikua jumla 289 yenye washiriki 14,110
mafunzo haya yalitengeneza ajira mbalimbali 56,440.
MTAWANYO WA MAFUNZO YALIYOTOLEWA KWA KILA
MWAKA NI KAMA IFUATAVYO:-
NA MWAKA IDADI YA
MAFUNZO
IDADI YA WANUFAIKA
1 2016 42 2,680
2 2017 18 600
3 2018 37 1,398
4 2019 36 1,832
5 2020 40 1,650
6 2021 51 4,420
2022 45 850
2023 20 680
JUMLA
IV. UTOAJI WA MIKOPO KUPITIA MFUKO WA WAJASIRIAMALI
WADOGO WANANCHI.
Kupitia mfuko wa wajasiriama wadogo Wananchi (NEDF) tuliendelea
kushughulikia maombi na kutoa mikopo midogo ya uwekezaji na mitaji
geugeu yenye thamani ya Tshs 493,100,000/=kwa wajasiriamali 178
katika kipindi cha mwaka 2016 hadi 2021.
MTAWANYO WA MIKOPO ILIYOTOLEWA KATIKA MWAKA NI
KAMA IFUATAVYO:
NA MWAKA IDADI THAMANI
1 2016 43 110,700,000/=
2 2017 27 64,400,000/=
3 2018 26 47,700,000/=
4 2019 21 49,000,000/
5 2020 30 109,000,000/=
6 2021 31 112,300,000/=
7 2022 31 110,300,000/=
8 2023 35 129,000,000/=
JUMLA 244 732,400,000/=
Mheshimiwa Naibu Waziri;
6.0 Ili kutekeleza kikamilifu mipango ya maendeleo na Ilani ya CCM
vinavyokusudia kuleta mapinduzi ya viwanda kwa kuanzisha viwanda
vinavyozalisha bidhaa muhimu kwa wananchi kwa kutumia malighafi
zinazopatikana nchini na kutumia nguvukazi kubwa( light manufactures);
SIDO Mbeya tunayo mikakati ya kusukuma dhamira hii ya serikali na
chama tawala kwa njia tatu:-
 Kuendelea na kuhamasisha mkakati wa unzishwaji viwanda kwa mfumo
wa kongano (Industrial Clusters Strategy), hii tumedhamiria iwe katika
ngazi ya wilaya kutegemeana na malighafi au rasilimali zilizopo katika
wilaya na zinazopatikana kwa wingi katika wilaya husika. Mfano Ileje
kongano la Alzeti , Kyela kongano la mafuta ya mawese, Mbalali kongano
za uchakataji mpunga nk. Njia hii itawezesha kuanzishwa viwanda kwenye
maeneo yaliyotengwa na Halmashauri za wilaya , na hivyo kuwezesha
wadau kutoa huduma zinaziostahili na wajasiriamali, kuwezesha
kutengeneza mtandao wa mawasiliano,kuchangia rasilimali, kuongeza
ubunifu na kubadilishana maarifa .
 Mkakati wa Wilaya Moja Bidhaa Moja. Mkakati huu unalenga kuchagua
zao moja ambalo litapewa msukumo zaidi kwenye uzalishaji katika wilaya
ili kuleta maendeleo ya viwanda na kuongeza ajira kwa vijana hasa vijana
wanaomaliza vyuo ili wasibaki mijini bali warudi vijijini wakasaidie ukuzaji
wa uchumi.
 Kuendeleza program ya kitamizi; Mpango huu unalenga kuibua mawazo
ya ubunifu ya teknolojia, bidhaa na miradi , hususani kwa vijana
wanaomaliza vyuo .SIDO Mbeya tunalo jengo lenye vyumba ambavyo
vimetengwa kwa madhumuni hayo lakini ukarabati haujakamilika hasa
upande wa miundombinu stahiki . Mpango huu utawezesha kuanzisha
miradi yenye ufanisi na kuleta bidhaa mpya kwenye soko.
Mheshimiwa Naibu Waziri,
7.0 Pamoja na utendaji tuliouelezea na mikakati tuliyonayo zipo
changamoto ambazo kwa kiasi hurudisha nyuma ufikiwaji wa
malengo kama inavyoweza kuwa imekusudiwa . Miongoni mwa
changamoto hizo ni kama ifuatavyo:-
 Upatikanaji wa maeneo ya kuanzisha kongano/ kombania za viwanda
, na tukiyapata yanahitaji gharama za utwaaji, fidia na upimaji . Mfano
Mbeya vijijini, Momba, ileje na mbozi maeneo yanapatikana lakini
yanahitaji fidia.
 Ufinyu wa bajeti husababisha kutofikisha shuguli zetu kwenye vijiji
pamoja na kuwa mahitaji ni makubwa sana.
 Bado fedha za mfuko wa wajasiriamali wadogo wananchi (NEDF) ni
kidogo sana kutuwezesha kutimiza matakwa ya wajasiriamali wadogo
na wa kati na hasa kutoa fedha hizo kwenye maeneo ya vijijini hasa
wilayani na kuwa na ufanisi.
 Kutokua na usafiri wa kutosha kufanya huduma za ugani, Magari
tunayotumia ni ya mwaka 2002 , magari haya ni machakavu ,
yanahitaji ukarabati wa mara kwa mara ambao una gharama kubwa
sana.
 Tunayo karakana ambayo ina buni na kutengeneza mashine na
mitambo mbalimbali, kutengeneza vipuri na kukarabati mitambo katika
viwanda ili kuchochea uanzishwaji na uendelezaji wa viwanda vidogo
lakini inakabiriwa na upungufu mkubwa wa watumisha hali
inayopelekea kazi za wateja kuchelewa wakati mwingine.
 Ofisi ya Mkoa kutokidhi mahitaji,ofisi tunayotumia ni ndogo hivyo
hulazimu wafanyakazi wengine kufanya kazi katika ukumbi wa
mafunzo ambao nao hutumiwa kuwahudumia wateja wanaokuja
kufanya malipo ya vibanda ,hii inatokana pia na wingi wa wapangaji
hivyo baadhi ya ofisi zinatumika kutunza mafaili ya wateja.
Mheshimiwa Naibu Waziri;
8.0 Mwisho, Bado nasisitiza na kuomba kuwa mkakati wa uanzishwaji wa
viwanda kwa mfumo wa kongano (cluster Industrial Development
Approach) utengewe bajeti ya serikali na iwe ni agenda ya kudumu
kwenye vikao katika ngazi zote na kwenye wizara za kiuchumi. Maana
kongano hizi ndizo zitawezesha serikali kutoa misaada, kutakua na
urahisi wa kuhawilisha teknolojia,itawezesha kuimarisha maarifa ya
wazalishaji,wadau mbalimbali watatoa huduma kwa wanaviwanda
wakiwa pamoja na kuongeza ufanisi wa uzalishaji. Na hivyo kutimiza
azma ya ujenzi wa msingi wa viwanda katika ngazi za mikoa na taifa kwa
ujumla. Aidha tunashukuru kwa jitihada zinazoonekana za kutuongezea
nyenzo za utendaji kazi lakini bado tunaomba tupate msaada wa magari
ili kuongeza kasi ya utendaji kazi tulizojipangia kwenye mkakati wetu na
mipangokazi.
Kaimu Meneja Mbeya SIODO, akisisitiza jambo baada ya kumaliza kusoma hotuba yake

Naibu Waziri Kigahe, akizungumza na uongozi wa SIDO mkoa wa Mbeya ,kabla ya kuanza safari kukagua mitaa mamnelele



Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA