Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akutana na Kuzungumza na Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn, Dakar Senegal
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2023/01/0F442C24-266D-453E-A6A4-4F0F10BE5C37-860x384.jpeg)
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na
Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn ambaye pia ni Mwenyekiti wa Africa’s Food Systems Forum (AGRF) mara baada ya mazungumzo yao Dakar, Senegal tarehe 26 Januari, 2023.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa
kwenye picha ya pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia Mhe.
Hailemariam Desalegn pamoja na ujumbe wake mara baada ya mazungumzo
Dakar nchini Senegal tarehe 26 Januari, 2023. wengine katika Picha ni
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe pamoja na Viongozi wengine kutoka Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa pamoja na Marais wa nchi mbalimbali za Afrika wakati akizungumza
kwenye Mkutano wa Kilimo na Chakula kwa Bara la Afrika uliofanyika
Dakar nchini Senegal.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn aliyeambatana na ujumbe wake Dakar, Senegal tarehe 26 Januari,2023. Pamoja na mambo mengine, katika kikao hicho wamezungumzia jinsi ambavyo Tanzania imejiandaa kuwa mwenyeji wa Mkutano mkubwa wa Kilimo utakaohusisha, viongozi, watu mashuhuri na Wadau wapya 3,000. Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn ni Mwenyekiti wa Africa’s Food Systems Forum (AGRF)
Comments
Post a Comment