WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf
Mkenda,akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 17 wa Umoja wa Wakuu
wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA) unaofanyika jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) anayeshughulikia
Elimu Dkt. Charles Msonde,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 17 wa
Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA) unaofanyika
jijini Dodoma.
Rais wa Umoja wa Wakuu wa Shule
za Sekondari Tanzania (TAHOSA), Frank Mahenge,akisoma risala wakati wa
Mkutano Mkuu wa 17 wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania
(TAHOSSA) unaofanyika jijini Dodoma.
SEHEMU ya Washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,(hayupo pichani) wakati
akifungua Mkutano Mkuu wa 17 wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari
Tanzania (TAHOSSA) unaofanyika jijini Dodoma.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf
Mkenda,akiagana na Walimu mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 17 wa
Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA) unaofanyika
jijini Dodoma.
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,
imewataka walimu wote nchini kuzungumza na wanafunzi kuhusu masuala ya
malezi kwa kuwa wao hukaa muda mrefu na wanafunzi ili kukuza kizazi
chenye maadili bora.
Hayo yamesemwa leo Desemba 15,2022 jijini Dodoma Wakati
akifungua Mkutano Mkuu wa 17 wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari
Tanzania (TAHOSSA),amesema kuwa walimu ni muhimu sana kwa maendeleo ya
taifa hivyo watumie nafasi zao kuandaa kizazi chenye weledi.
Waziri Mkenda ametaka walimu kufuata
muongozo wa malezi kwa kusimamia kikamilifu suala la maadili kwa
Wanafunzi ili kukuza kizazi chenye maadili bora kwa Maendeleo ya Taifa.
“Natoa onyo kali kwa walimu wachache
wenye tabia mbaya zinazochafua sura ya walimu katika jamii, serikali
itaendelea kuwashughulikia walimu wenye mwenendo mbaya na kuwachukulia
hatua kauli za kisheria,”amesema Prof.Mkenda
Aidha amesema kuwa
hataki kuona wanafunzi wanalala kitanda kimoja na kama kuna changamoto
ya vyoo pia pigeni simu kwa Mkurugenzi mueleze changamoto hizo lengo ni
kuhakisha mazingira salama ya utoaji elimu na kuwalinda watoto.
Kuhusu kuvuja kwa mitihani,Waziri
Mkenda amesema kuwa kuna baadhi ya walimu wamekuwa na tabia isiyofaa
ya kushiriki katika kuvujisha na kusambaza mitihani kwa wanafunzi kwa
maslahi yao binafsi au kupandisha hadhi ya shule ionekane ina ufaulu
mzuri.
“Niwaonye walimu wa namna hii kuacha
tabia hii na badala yake wafanyekazi kwa weledi na ubunifu ili
kuwasaidia wanafunzi kupata maarifa na kufaulu vizuri kwenye mitihani
yao,”amesisitiza
Hata hivyo amewataka Walimu kuangalia maudhui ya vitabu
vinavyoingia shuleni ili visiharibu wanafunzi lakini pia kutumia Skauti
na Viongozi wa dini katika kuendeleza malezi mazuri ya watoto shuleni.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Dkt.
Charles Msonde amewataka Wakuu wa Shule kufuatilia utendaji wa walimu
shuleni ili kuondoa alama F kwenye masomo wanayofundisha.
Awali Rais wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania
(TAHOSA), Frank Mahenge ameishukuru Serikali kwa namna inavyoshirikiana
na Umoja huo na kuiomba pamoja na kazi nzuri wanayoifanya ya kuboresha
mazingira ya utoaji wa elimu nchini.
Comments
Post a Comment