SERIKALI YAMPONGEZA MWEKEZAJI WA KILIMO MKOANI KAGERA

 

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo Dkt.Sophia Kashenge akitazama shamba la ngano la Mkuu wa Kampuni ya Global Agency ltd  ililopo mkoani Kagera

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Global Agency ltd  Fidelis Bashasha akitoa maelezo mbele ya viongozi wa Taasisi za Wizara ya Kilimo ASA,TOSCI na TARI kwa kukagua na kutembelea Shamba hilo kubwa la Mbegu.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Global Agency ltd  Fidelis Bashasha akisisitiza jambo mbele ya viongozi hao

Shamba kubwa la Mbegu ya ngano la Kampuni ya Global Agency ltd  .

@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@


Mkurugenzi wa Mazao wa Wizara ya Kilimo  Nyasebwa Chimwagu amelidhishwa na Mwekezaji wa Mzawa wa Kampuni ya Global Agency ltd inayojihusisha na Uzalishaji wa Mbegu za kilimo Mkoani Kagera.

Akizungumza na waandishi wa Habari Nyasebwa Chimwagu katika Shamba la Kampuni hiyo lililopo katika Kijiji Cha Buchurago Mkoani Kagera amesema serikali imelidhishwa na utendaji kazi wa mwekezaji huyo ambao umelenga kuongeza Uzalishaji wa Mbegu kwa kiasi kikubwa.

Chimwagu akiwa ameongozana na wataalam wa kilimo kutoka Taasisi za ASA,TARI na TOSCI amesema serikali itaendelea kushirikiana bega kwa bega na sakta Binafsi katika sekta ya kilimo ilikuongeza tija Uzalishaji wa Mbegu hasa katika nyakati hizi za uhitaji wa Mbegu za kilimo ni mkubwa.

Amesema Kampuni hiyo imeenda mbali zaidi na kuweka miundombinu ya Umwagiliaji wa kisasa hali ambayo inawafanya wazalishe Mbegu kwa misimu yote pasipo kutegemea Mvua.

Kwaupande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo Dkt.Sophia Kashenge amesema Wakala utafanya kazi na Kampuni ya Global Agency ltd kwa kuzalisha Mbegu za kilimo.

Amesema kwa kuanza wataanza na Uzalishaji wa Ngano ambapo katika Shamba hilo Ngano inafanya vizuri kulingana na majaribio yaliyofanywa hivi Karibuni.

Dkt.Sophia ameipongeza Kampuni hiyo Kwa uwekezaji mkubwa wa kisasa katika sekta ya miundombinu ya Umwagiliaji ambayo inawafanya wafanye kazi Kwa mwaka Mzima.

Kwa upande wake Afisa Mfawidhi wa Taasisi ya uthibiti Ubora wa Mbegu za kilimo (TOSCI) Joseph Ngura amesema Kampuni hiyo wamekuwa wakishirikiana nao katika hatua mbalimbali za Uzalishaji wa Mbegu nakujilidhisha Uzalishaji wa Mbegu zote unafuata taratibu zote zilizowekwa.

Ngura amesema TOSCI wataendelea kufanya kazi vizuri na sekta binafisi Ili ufanisi wa kazi zao uwe bora hali ambayo itaongeza thamani ya Mbegu hizo.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Global Agency ltd  Fidelis Bashasha ameipongeza serikali kwa Kutuma viongozi wa Taasisi za Wizara ya Kilimo ASA,TOSCI na TARI kwa kukagua na kutembelea Shamba hilo kubwa la Mbegu.

 Ameipongeza serikali kwa kuwatambua wawekezaji wa ndani na kuwapa fursa za Uzalishaji wa Mbegu ambazo zitatumika Nchini.

Bashasha ameipongeza Taasisi ya Wakala wa Mbegu za kilimo ASA kwa kufika shambani nakujione Uzalishaji unavyoendelea wa Mazao ya mahindi na Soya.

Amesema kama sekta binafisi wataendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha sekta ya kilimo inakuwa Zaidi.

Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA