WAZIRI MKENDA ATANGAZA TUME YA MIKOPO KWA WANAFUNZI ELIMU YA JUU
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akitangaza tume ya kuchunguza utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu tarehe 29 Julai 2022 Jijini Dar es laam wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini juu ya mwelekeo wa Wizara, Vipaumbele na maeneo ya kimkakati katika utekelezaji kwa Mwaka wa fedha 2022/23. Na Mathias Canal, WEST Wakati dirisha la maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2022/2023 likiwa wazi kwa muda wa siku 70 kuanzia Julai 19 hadi Septemba 30 mwaka huu, Serikali imetangaza Tume ya watu watatu kuchunguza utoaji wa mikopo. Tume hiyo itaongozwa na Prof Allan Mushi ambaye ni mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro, Idd Makame kutoka Zanzibar na Dkt Martin Chegeni ambao wote kwa pamoja ni wataalamu wa mifumo waliobobea katika sayansi ya Kompyuta na Takwimu. Tume hiyo itachunguza uhalali katika utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2017/2018 mpaka 2021/2022 ili kubaini kama kulikuw