Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yapitishwa na Bunge
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisoma hotuba ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019 bungeni jijini Dodoma. Mapema leo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepisha kiasi cha Shilingi Bilioni Mia Moja Sabini na Saba, Milioni Sita na Mia Mbili Thelathini na Mbili Elfu. Kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni Mia Moja Sitini na Sita, Milioni Mia Sita na Sita, na Mia Mbili Thelathini na Mbili Elfu ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida, na Shilingi Bilioni Kumi na Milioni Mia Nne ni kwa ajili ya bajeti ya maendeleo. Pro. Adolf F. Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,(wa kwanza kushoto) akifuatilia uwasilishwaji wa hotuba ya bajeti ya Wizara. Wa pili kutoka kushoto, ni Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhani Mwinyi akifuatilia hotuba. Sehemu ya Watendaji wa Wizara wakifuatilia hotuba ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/20