KONGAMANO LA MIAKA 17 KIFO CHA NYERERE

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwaongoza wageni wake kusimama wima kutoa mheshima kwenye kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, kabla ya kupokea misaada kwa ajili ya waathilika wa tetemeko mkoani Kagera. Hafla hiyo ilifanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo
Mwandishi wa Waziri Mkuu Irene Bwire Kakiziba, akiongoza kikao hicho cha kuchangia waathilika wa tetemeko mkoani Kagera
Waziri Mkuu, akipokea mchango kutoka kwa Mwenyekiti wa Wasanii tanzania Cassian Taalib
Akimpongeza 
Wanahabari, wakichukua matukio
Waziri Mkuu akipokeamhundi kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Muktasi TanzaniaZuhuru Songambele
 Waziri Mkuu, akipokea bango lenye mfano wa Hundi kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Madini tanzania Stamiko Zena Kongoro
 Waziri Mkuu, akizungumza katika hafla hiyo
Mzee Chilo akiomba duaa baada ya kumalizika hafla hiyo
 Akipiga picha ya pamoja na viongo\zi wa wasanii

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiagana na Kikumbi Mwanza Mpango (King Kikii), Baada ya kupokea misaada ya wanajumuiya ya wasanii nchini waliyoitoa kwa ajili ya waathilika wa tetemeko mkoani Kagera
Akiagana na mzee Chilo
 Akipiga picha ya pamoja na wamachinga baada ya ku[pokea misaada
Picha ya pamoja na makatibu muktasi

 Picha ya pamoja na viongozi wa stamiko
Akiteta na Coletha Njerekela, ambaye ni Afisa Uhusiano wa Stamiko

Pichya ya pamoja na waandishi wa habari
 Wanahabari wakipiga picha nae waziri mkuu

Picha ya upendeleo ya wanahabari wa kike


 KONGAMANO LA MWALIMU NYERERE LEO KIGAMBONI
 Mmoja wa wachangiaji katika kongamano hilo akiwalaumu wanasiasa kujali matumbo yuao

 Profesa Samuel Wangwe, akichangia


DAR ES SALAAM     
MWENYEKITI wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, amesema kutokana na miiko iliyowekwa na mwasisi wa Taifa, Hayati Mwalimu Julias Nyerere, mtu yeyote anayekuwa rais wa nchi lazima atambue kuwa watu wote ni sawa na “usiwe wewe ni rais tembo.”
Hayo aliyasema jana wakati akiwasilisha mada ya miiko ya uongozi katika kongamano la kumbukizi ya  Mwalimu Nyerere lililofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Alisema kwa mujibu wa Katiba ya TANU ya mwaka 1954 imani ya chama ilikuwa binadamu wote ni sawa, kila mtu anastahili heshima na kwamba kila raia ni sehemu ya Taifa.
Alisema nchi ambayo mwalimu aliijenga ilikuwa na misingi ya “binadamu wote ni ndugu zangu” na kwamba hata alipokwenda nje ya Tanzania alirudia kuwa msingi wa kuendesha taifa letu na kushirikana na yeyeyote  wa umoja wa mataifa, utakuwa katika msingi wa imani ya usawa wa binadamu na yote yanayojenga usawa huo.
 “Tunachosema ni kwamba miiko ilikuwa inasema ukitaka kuwa rais utambue na uwe na imani kuwa watu wote ni sawa usiwe wewe ni tembo,” alisema Butiku na kuongeza:
“Lazima utambue kuwa unatokana nao (watu) na lazima kiongozi huyo atambue kuwa anaongoza watu hivyo anapaswa kuwaongoza kwa heshima.”
Alisema miiko ya uongozi ilikuwa kuwa viongozi lazima awe mkulima au mfanyakazi na asishiriki katika shughuli zozote za ubepari.
Aliongeza pia iliwataka viongozi kuchagua ama kuwa viongozi wa watu au viongozi wa kutafuta utajiri na kwamba wanasiasa wengi wamekuwa wakipingana na kanuni hiyo.
 “Katika siasa za hivi sasa wanasiasa wote wanajitahidi sana kukataa kanuni hii na wamekuwa wakibabaisha. Msibabaishe,” alisisitiza Butiku.
Mada ya miiko ya uongozi pia iliwasilishwa na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Wilson Mkama, ambaye  alijikita katika kuelezea dhana ya uongozi ambapo alibainisha kuwa viongozi lazima wapatikane kwa haki na uwazi.
Alionya kuwa ni hatari kwa viongozi kupatikana kwa njia za vitisho, ujanja, ulaghai na rushwa na kwamba kufanya hivyo ni kupoteza sifa za uongozi.
 “Asili ya uongozi ni watu na viongozi lazima wapatikane kwa haki na uwazi na si kwanjia za ujanja ujanja, vitisho, ulaghai na rushwa na iapokuwa hivyo tunapoteza sifa ya uongozi,” alisema Mkama.
Akipongeza dhana ya Rais MAgufuli ya Hapa Kazi tu alisema kiongozi lazima afanye kazi kwa kufuata utaratibu wa kisiasa uliowekwa.
“Watu wamekuwa wakitafsiri siasa vibaya lakini ukweli ni kwamba siasa ni namna ya kutengeneza utaratibu wa maisha na maamuzi ya kisisa ndio yanayoijenga jamii,” alisisitiza.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) bara, Philip Mangula, ambaye aliwasilisha mada ya viongozi na maadili alisema kwa kiasi kikubwa chama chake kimekuwa kikizingatia maadili ya viongozi.
Alisema kwa sasa chama hicho chini ya Mwenyekiti wake Rais John Magufuli kinahakikisha kinatokomeza rushwa serikalini na katika chama hasa wakati wa uchaguzi.
“Katika mkutano Mkuu wa mwaka 2012 ambao ndio ulinichagua kuwa makamu mwenyekiti na nikapata uenyekiti wa kamati ya maadili, tuliazimia kuchukua hatua haraka kwa viongozi wala rushwa na ndio kazi anayofanya Rais Magufuli,” alisema Mangula.
Mangula ambaye amepewa jina la utani la mzee wa mafaili kutokana na staili yake ya kupitia mafaili ya wanachama wanaotaka uongozi, alisema mafaili bado yanaendelea kurekodiwa na mwisho yatafunguliwa kwa kila atayetaka uongozi.
Alionya kuwa wapo watu ambao wameshaanza kutoa zawadi na misaada bila kuzingatia taratibu za chama kwa lengo la kutengeneza mazingira ya kupata uongozi katika uchaguzi ujao na kusisitiza kwamba “safari hii imekula kwao.”
Kauli hiyo ya Mangula inaunga mkono vita iliyotangazwa na Rais Magufuli siku ayokabidhiwa mikoba ya Uenyekiti wa chama hicho mjini Dodoma.
Rais Magufuli alitangaza kufanya mapinduzi makubwa ya kimfumo ndani ya CCM ikiwa ni pamoja na kukomesha uongozi unaopatikana kwa njia ya rushwa.
Magufuli ambaye amekuwa akijinasibu kupambana na rushwa na ufisadi alikitaja waziwazi chama hicho kama moja ya taasisi zinazotajwa kuongoza kwa rushwa licha ya kukatazwa katika ahadi ya tatu ya CCM pamoja na kifungu cha 18 cha Katiba ya CCM.
 “Niligombea urais niliyaona huko Iringa wakati wa kutafuta wadhamini, Wilaya yote ilikuwa imenunuliwa ilibidi nisafiri kwenda ndani huko vijijini. Fedha imekuwa kigezo cha mtu kupata uongozi…ukitaka urais kiasi fulani, ubunge kiasi fulani, diwani kiasi fulani. Tumekuwa tukipoteza sehemu zingine kuchagua wenye pesa badala ya anayekubalika,” alisema Magufuli. 
Alisema amedhamiria kukomesha jambo hilo na kwamba mtu atakayetoa rushwa hatachaguliwa wala kupitishwa kwa mujibu wa kanuni ambazo alikabidhiwa jana na Mwenyekiti mstaafu.

Mangula na Butiku wakiwa katika kongamano hilo
 Spika mstaafu Anne Makinda, akiongoza mdahalo wa kumbukumbu ya mwalimu Nyerere iliofanyika  Kigamboni Da es Salaam  jana. Kulia ni Ibrahim Kaduma na katikati ni Willison
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo
Profesa Lipumba nae alikuwepo


Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA