NAPE AVIFUNGIA VITUO VYA REDIO DAR NA ARUSHA
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akitoa tamko la kufungia vituo viwili vya redio ambavyo ni Kituo cha Redio Five Arusha na Magic FM Dar es Salaam kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, kutokana na kukiuka Kanuni za Sheria ya Utangazaji ya mwaka 2005 kwa kurusha hewani vipindi vyenye maudhui ya uchozezi,na Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Uratibu wa Vyombo vya Habari Bw. Jamal Zuberi wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo. Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia tamko alilokuwa akitoa Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (hayupo pichani) la kufungiwa kwa Redio Five Arusha na Redio Magic FM Dar es Salaam leo Agosti 29,2016 Jijini Dar es Salaam. Serikali yafungia vituo viwili vya redio nchini kutokana na kurusha hewani taarifa za kichochezi zinazoweza kuchangia uvunjifu wa amani. Tamko la kufungwa kwa vituo hivyo vya redio limetolewa leo Jijini