Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunga "Zoezi la Onesha Uwezo Medani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi wa Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha waliojitokeza kumsalimia wakati akielekea Monduli kwa ajili ya kufunga zoezi la Onesha uwezo Medani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Mbauda Mkoani Arusha hawaonekani pichani wakati akielekea Monduli kwa ajili ya kufunga zoezi la Onesha uwezo Medani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisoma bango mara baada ya kukabidhiwa na mwananchi mmoja katika eneo la Kona ya Nairobi Mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Arusha katika eneo karibu na chuo cha Arusha Tech. Wananchi hao walifunga barabara ili wapate nafasi ya kumuona Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Mianzini Mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis Mwamunyange wakati waufungaji wa zoezi la Onesha Uwezo Medani lililofanyika Monduli nje kidogo ya Jiji la Arusha.
Wakibadilishana mawazo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa jeshi katika tukio hilo la Ufungaji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kwenye uwanja wa maonesho akiwa pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis Mwamunyange.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa ngazi za juu wa Jeshi mara baada ya kufunga zoezi la Onesha Uwezo Medani Monduli Mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akishuhudia matukio ya zoezi la Onesha Uwezo Medani Monduli Mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akipewa maelezo ya zana mojawapo ya Kivita katika Zoezi la
Onesha Uwezo Medani Mkoani Arusha. Picha
na IKULU
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI
YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunga "Zoezi la Onesha
Uwezo Medani" lililoandaliwa na kutekelezwa na Kamandi ya Jeshi la Nchi
Kavu ambalo ni sehemu ya Jeshi la wananchi Tanzania katika eneo la Lang'arurusu
nje kidogo ya Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha.
Akizungumza na
Askari na Maafisa wa Jeshi la wananchi Tanzania kabla ya kufunga zoezi hilo, Rais
Magufuli amesema katika awamu yake ya tano ya uongozi amedhamiria kulitumia
Jeshi la wananchi Tanzania katika kujenga uchumi, ikiwemo kuanzisha viwanda na
kampuni za ujenzi ili kuharakisha maendeleo.
Ametoa mfano wa
kiwanda cha Nyumbu ambacho kipo chini ya jeshi la wananchi Tanzania na kueleza
kuwa wakati umefika wa kukiimarisha na kukiendeleza kiwanda hicho, ili kiweze
kufanya uzalishaji mkubwa kwa manufaa ya nchi ikilinganishwa na hali ilivyo
hivi sasa.
"Zipo nchi
nyingi ambazo majeshi yao yanatumika katika uchumi na yanafanya kazi nzuri ya
kupigiwa mfano, wakati umefika na sisi kufanya hivyo. Hata hizi sare za jeshi
na viatu, hatuna sababu ya kuvinunua kutoka nje ya nchi, tunaweza kutengeneza
sisi wenyewe" Alisisitiza Rais Magufuli.
Rais Magufuli
amelipongeza Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kuandaa "Zoezi
Onesha Uwezo Medani" ambalo limethibitisha uwezo, weledi na utayari lilionao
katika jukumu lake la kiulinzi.
Ameahidi kuwa
ataendeleza juhudi zilizofanywa na viongozi wenzake waliotangulia za kuliimarisha
kwa vitendea kazi na maslai ya wanajeshi ili liweze kutekeleza wajibu wake bila
vikwazo.
Pamoja na
kuwapongeza Askari na maafisa wa Jeshi la wananchi Tanzania walioshiriki katika
zoezi hilo, Rais Magufuli ameagiza Askari Mgambo na Askari wa Jeshi la kujenga
Taifa (JKT) walioshiriki zoezi hilo kuajiriwa na jeshi la wananchi Tanzania.
Akitoa maelezo ya
awali kabla ya hotuba ya Rais Magufuli, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Wizara yake itaongeza na kusimamia
juhudi za kuliboresha jeshi hilo kwa zana, vifaa na maslai kwa wanajeshi ili
kuwajengea uwezo na morali ya kutekeleza majukumu yao ya kuilinda nchi, pamoja
na kutoa msaada stahiki kwa nchi zenye kuhitaji ulinzi wa amani popote duniani.
Kwa upande wake
Mkuu wa majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Adolf Mwamunyange
amemhakikishia Rais Magufuli kuwa Jeshi la wananchi Tanzania lipo imara na
litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi, nidhamu ya hali ya juu na
uzalendo mkubwa.
Kabla ya
kuwahutubia maafisa wa jeshi la wananchi, Askari na wananchi waliohudhuria
ufungaji wa "Zoezi Onesha Uwezo Medani", Rais Magufuli ameoneshwa
zana mbalimbali za kivita ikiwa ni pamoja na kushuhudia upigaji wa mizinga ya
masafa mafupi, masafa ya kati na masafa marefu.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Arusha
22
Januari, 2016
Comments
Post a Comment