KILANGO ATEMBELEA CHUO CHA UFUNDI STAD CHAN'OMBE DAR
Mkufunzi wa
Chuo cha VETA cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)-Kipawa, Bw.
Abdul Mollel (kulia) akimuonesha na kumuelezea Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo
ya Ufundi, Mh Anna Kilango Malecela, nyenzo na mifumo mbalimbali inayotumika
kufundishia wanafunzi katika chuo hicho. Naibu Waziri Anna Kilango Malecela
alitembelea Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ikiwa ni pamoja
na Vyuo vya vinavyomilikiwa na VETA vilivyopo jijini Dar es Salaam siku ya
Jumanne, 21 Aprili, 2015.
Rhoda Mbwanji Mwanafunzi wa
Kozi ya Wasaidizi wa Maabara inayotolewa na Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Stadi na Huduma Dar es Salaam-Chang’ombe,
(kushoto),
akimuonesha Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Anna Kilango
Malecela (wa pili kushoto) namna ya kuchanganya kemikali kwa ajili ya mahitaji
mbalimbali wakati Naibu Waziri alipotembelea Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Stadi (VETA) Jumanne, 21 Aprili, 2015. Wengine kutoka kushoto ni Mratibu
wa Mafunzo, VETA kanda ya Dar es Salaam, Bi. Florence Kapinga, Kaimu Mkurugenzi
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Thomas Katebalirwe, Mkufunzi wa Chuo cha
VETA Dar es Salaam Henry Maseko na Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah
Moshi.
Comments
Post a Comment