Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa akiwasilisha mada juu ya umuhimu wa mawasiliano ya kimkakati kwa Maafisa habari wa Serikali katika Kikao kazi cha 20 cha Maafisa habari hao kinachoendelea katika Ukumbi wa Hoteli ya Amaan, Zanzibar leo tarehe 4 Aprili 2025 Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amesema mada mbalimbali zitakazojadiliwa katika Kikao kazi cha 20 cha Maafisa Habari, Uhusiano, Mawasiliano na Itifaki wa Serikali, zitawaongezea uelewa na mbinu za kisasa za kutangaza shughuli za serikali pamoja na namna bora ya kukabiliana na upotoshaji unaofanywa kwa makusudi na baadhi ya watu. Mhe. Prof. Kabudi ameyasema hayo Aprili 3, 2025 wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi cha 20 cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki kilichofunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla katika ukumbi wa New Amaan Hotel Zanzib...