Posts

WAZIRI SILAA ASIMAMISHA MATUMIZI YA KITUO CHA MAFUTA CHA BARREL DAR ES SALAAM

Image
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa akiozungumza na wananchi wa Mikocheni wakati akisimamisha matumizi ya Kituo cha Mafuta cha Barrel Petrol Energy cha Mikocheni Desemba 23, 2023 jijini Dar es salaam. . Mwakilishi wa Kituo cha Mafuta cha Barrel Petrol Energy cha Mikocheni Mhandisi Stanley Kitundu akizungumza na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa (hayupo pichani) kwa niaba ya mmiliki wa kituo hicho ambacho kimesimamishwa kutoa huduma 23, 2023 jijini Dar es salaam   Na Eleuteri Mangi, WANMM   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amesimamisha matumizi ya Kituo cha Mafuta cha Barrel Petrol Energy cha Mikocheni jijini Dar es salaam na kupiga marufuku ujenzi holela wa vituo vya mafuta nchi nzima vinavyojengwa kwenye makazi ya watu hatua inayohatarisha usalama wa watu na mali zao.   Waziri Silaa ametoa agizo hilo Desemba 23, 2023 alipoenda kukagua eneo kilipojengwa kituo hicho na ...

NEEMA YA MISAADA YAZIDI KUWAFIKIA WAATHIRIKA WA MAAFA HANANG’

Image
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi akikabidhi misaada kwa Waathirika wa maafa ya Hanang Leo Desemba 23, 2023 kwa mara ya tatu na wengine zaidi katika kituo cha Shule ya Msingi Gendabi.  Waathirika wa maafa ya Hanang wakipokea misaada jana Desemba 23, 2023 kwa mara ya tatu na wengine zaidi katika kituo cha Shule ya Msingi Gendabi. @@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@ Na Mwandishi wetu, Hanang Waathirka wa maafa yaliyotokea wilayani Hanang mkoa wa Manyara, Desemba 3, mwaka huu, wameendelea kunuifaika na misaada mbalimbali ya kibinadamu iliyotolewa na wadau pamoja na serikali, baada ya serikali kuongeza kiwango cha ugawaji wa misaada kwa kaya kutokana na ongezeko la misaada inayoendelea kupokelewa kutoka kwa wadau. Awali, serikali ilikuwa ikiwagawia waathirika hao misaada muhimu kama unga, mchele, unga wa ngano, mafuta ya kupikia, sukari, chumvi, maharagwe ya kuwatosheleza kwa kipin...

MUSOMA VIIJIJINI WAENDELEA KUJENGA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI KWENYE SEKONDARI ZAKE ZA KATA

Kwenye miradi ya ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi (fizikia, kemia na bailojia) kwenye Sekondari zetu za Kata, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo anashirikiana na: (i) Serikali yetu, (ii) Wanavijiji  (iii) Wadau wa Maendeleo na (iv) Baadhi ya Wazaliwa wa Musoma Vijijini Maabara za Etaro Sekondari: Sekondari hii ni moja ya Sekondari 25 za Kata za Jimbo la Musoma Vijijini. Ilifunguliwa Mwaka 2006 na hadi sasa maabara zake ni hizi zifuatazo: (i) Maabara ya Bailojia - imekamilika na itatumiwa (ii) Maabara ya Kemia - itakamilishwa kabla ya tarehe 15.1.2024. Serikali imechangia Tsh milioni 30 (iii) Maabara ya Fizikia - boma limekamilika kwa michango ya fedha na nguvukazi za wananchi wa Kata ya Etaro. Harambee ya leo ni ya kukamilisha ujenzi wa Maabara ya Fizikia kabla ya tarehe 30.1.2024 Michango ya wananchi ni: *Tsh 850,000 (zikiwemo za Walimu Makada wa CCM wa Kata ya Etaro, Tsh 42,000) *Saruji Mifuko 3. Michango ya Mbunge wa Jimbo ni: *Saruji Mifuko 100...

NAIBU WAZIRI MKUU DKT. BITEKO ASHIRIKI ROMBO MARATHON; APONGEZA UBUNIFU WAKE

Image
📌Apongeza nia ya Marathon kuhifadhi Mazingira, kuimarisha huduma za kijamii 📌Asema Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi zinazoanzishwa na wananchi kujiletea maendeleo na kukuza Utalii Rombo - Kilimanjaro Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo ameshiriki mashindano ya Rombo Marathon yaliyohusisha mbio za Kilometa tano, kumi na 21 na kupongeza waandaaji kwa ubunifu wao uliopelekea marathon hiyo kuendelea kuimarika kila mwaka ambapo licha ya kulenga katika kuimarisha afya kwa washiriki, imejikita katika kuchangia uboreshaji wa huduma mbalimbali za kijamii na utunzaji wa mazingira. Dkt. Biteko ametoa pongezi hizo tarehe 23 Desemba, 2023 wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, akiwa ni mgeni rasmi katika  marathon hiyo  ambapo alikimbia kwa umbali wa kilometa Tano akiambatana viongozi mbalimbali wa Kitaifa, Mkoa na Wilaya. "Nimeelezwa kwamba lengo la Rombo Marathon  ni kuhamasisha utunzaji wa mazingira, kukuza utalii wa ndani, kuchangia fedha kwa aji...