Posts

SERIKALI YAISHUKURU AfDB KUKUBALI KUFADHILI MIRADI YA UJENZI WA BARABARA NA USAFIRISHAJI WA UMEME

Image
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam Waziri wa Fedha na Mipango ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kukubali kuendelea kufadhili miradi ya maendeleo ya kipaumbele hususani ya ujenzi wa barabara na usafirishaji wa umeme ili kufungua fursa za kiuchumi katika kanda ya Magharibi. Dkt. Mpango ametoa shukrani hizo alipokutana na Wakurugenzi Watendaji 12 wanaowakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), jijini Dar es salaam. Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) ameiomba Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuharakisha kazi za upembuzi yakinifu na hatimaye kutoa fedha ili utekelezaji wa miradi ya Maendeleo kuanza mapema iwezekanavyo. Amesema kuwa Benki hiyo iliahidi kutoa fedha ili kujenga barabara ya Nyakanazi, kupitia Kibondo, Kasulu hadi Manyovu, kwa kiwango cha lami na kwamba mradi huo ukipatiwa fedha na kukamilika kwa wakati kutasaidia kuchochea biashara ya wakazi wa maeneo hayo na Nchi jirani ya Bur...

MATUKIO LEO

Image
Kulia Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustin Kamuzora, akitoa Tamko la Siku ya Mazingira Afrika kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Mkamba, Leo katika mkutano na waandishi wa Habari Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira wa Ofisi hiyo Bw. Richard Muyungi. TAMKO LA WN-OMR – MMZ BW. JANUARY Y. MAKAMBA KWA VYOMBO VYA HABARI. MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA AFRIKA TAREHE 3 MACHI, 2017 Ndugu Wananchi, Tarehe 3 Machi kila mwaka watanzania wote huungana na nchi nyingine za Afrika katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Afrika, ambayo huadhimishwa barani Afrika kila mwaka. Siku hii imetengwa kwa lengo la kukumbuka umuhimu wa kutunza na kuhifadhi mazingira barani Afrika. Azimio la kuadhimisha Siku hii lilipitishwa na kuamuliwa na Baraza la Mawaziri wanaosimamia Mazingira wa nchi za Afrika kwenye mkutano uliofanyika Durban, Afrika Kusini Mwaka 2002...