Airtel FURSA yawafungulia masoko mapya wajasiliamali wadogo wadogo jijini
Mkuu wa wilaya ya Kindondoni Mh Aly Hapi akikagua na kujionea bidhaa za mjasiliamali aliyewezeshwa na Airtel FURSA Bi Betty Mngulwi mwisho mwa wiki ambapo Airtel iliwakutanisha baadhi ya wajasiliamali jijini Dar es salaam katika maonyesho maalum ya ‘Airtel FURSA Wajasiliamali Bazaar’ nje ya ofisi kuu ya Airtel Morocco kwa lengo la kuwakutanisha wajasiliamali hao na wateja mbalimbali ili kuwatanua masoko yao na kuuza bidhaa zao. pamoja nae ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano wakwanza kulia. Mkuu wa wilaya ya Kindondoni Mh Ally Hapi akipokea zawadi ya keki toka kwa mjasiliamali aliyewezeshwa na Airtel FURSA Bi Diana Moshi mwishoni mwa wiki mara baada ya kutembelea banda la mjasiliamali huyo wakati wa maonyesho ya bidhaa za wajasiliamali katika maonyesho ya ‘Airtel FURSA Wajasiliamali Bazaar’ nje ya ofisi kuu ya Airtel Morocco yaliyoandaliwa na Airtel kwa lengo la kuwakutanisha wajasiliamali hao na wateja wa airtel il...