MATUKIO LEO
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akipata maelezo kuhusu uboreshwaji wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT),kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Prof. Zacharia Mganilwa alipokagua chuo hicho jijini Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akikagua moja ya darasa linalotumika kufundishia Marubani wa ndege alipokagua Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), jijini Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akiongea na wanafunzi wanaosoma kozi ya udereva alipotembelea Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), jijini Dar es Salaam. Kushoto (mwenye tai nyekundu) ni Mkuu wa Chuo hicho Prof. Zacharia Mganilwa. SERIKALI YAJIPANGA KUBORESHA SEKTA YA UCHUKUZI Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali imejidhatiti kufanya maboresho makubwa ya kimiundombinu na rasilimali watu katika sekta za uchukuzi ili kuiwezesh...