MOI SASA KIMBILIO LA WENGI ----------DKT MPOKI
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), Balozi Dkt Mpoki Ulisubisya , akizungumza leo na wanahabari katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dodoma, akisema Amelenga kuboresha huduma kwa kuanzisha mfumo wa miadi ya kidijitali ili kupunguza msongamano na kupendekeza huduma za saa 24. Aidha amebainishwa kwamba kuwahi foleni usiku wa maneno kwa ajili ya kutibiwa hivi sasa haipo mgonjwa anaweza kuweka ahadi na Daktari wake kwa kumpigia simu ukifika moja kwa moja unaenda kumuona, Hosptali ya moi imekuwa kimbilio la wengi tena baadhi kutoka nchi za nje. Amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha kutoa huduma hizo bora ambapo sasa wanaweza kumtibu mgoja wa kichwa bila kumpasua vifaa vingi vya kisasa vipo vya kutosha Huo ni uwezeshwaji wa Rais. Wanahabari wakichukua habari kutoka kwa Dkt Mpaki alipokuwa akizungumza nao