HAKUNA MTANZANIA ATAKAYEKOSA HUDUMA ZA UGONJWA WA UKIMWI WAZIRI MKUU MAJALIWA
WAZIRI Mkuu , Kassim Majaliwa, amewataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari kwa kuwa ugonjwa wa UKIMWI bado ni tishio na kiwango cha maambukizi mapya ni watu 60,000 kila mwaka ambapo vijana wanaopata VVU maambukizi ni takribani asilimia 34.3 ya maambukizi mapya. Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akisoma hotuba ya bajeti ya bajeti ya ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2025/26 na kusema kuwa Serikali itaendelea kuratibu shughuli za UKIMWI kwa kutoa huduma endelevu na stahimilivu kwa WAVIU. “Serikali itaendelea kuimarisha Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI ili uweze kufanikisha malengo ya nchi katika kutokomeza UKIMWI ifikapo 2030, kuweka msukumo katika kupunguza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto,kuhamasisha mabadiliko ya tabia katika jamii ili kupunguza maambukizi mapya ya VVU,”amesema. Sambamba na hayo, Serikali inatambua mabadiliko ya sera za misaada kutoka kwa baadhi ya wafadhili wa muda mr...