NAIBU WAZIRI WA KILIMO SILINDE AZINDUA MIRADI SAGCOT, AGRA JIJINI DODOMA
Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde amezindua Miradi itakayosaidia kuleta zaidi mageuzi katika Sekta ya Kilimo, inayofahamika kama SAGCOT: Support to SAGGOT Centre Ltd; na AGRA: Support to Tanzania’s Agriculture Transformation Office. Dhumuni la miradi hiyo ni kupanua wigo wa maeneo ya Kilimo Tanzania, yaani “The Agriculture Growth Corridors of Tanzania (AGCOT) kufuatia kusainiwa kwa mkataba wa makubaliano kati ya Norway na AGRA. Makubaliano hayo yamelenga kufungua vikwazo vya udhibiti wa kilimo ikiwa ni pamoja na vikwazo vya mauzo ya nje ili kuvutia uwekezaji wa Sekta Binafsi katika Sekta ya Kilimo nchini kupitia Ofisi ya Mageuzi ya Kilimo (Agricultural Transformation Office - ATO). Uzinduzi huo umefanyika tarehe 04 Februari 2025 jijini Dodoma na kuhudhuriwa pia na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Tine Tonnes; Mtendaji Mkuu wa Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT), Bw. Geoffrey Kirenga; Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ofis...