DKT. BITEKO AAGIZA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA TANESCO KUSUKWA UPYA
📌Akerwa na kusuasua kwa utendaji wa Kituo hicho 📌Awataka watendaji kuondokana na kufanya kazi kwa mazoea 📌Ahoji sababu za kutelekezwa kwa maelekezo yake ya 2024 Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishti Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameagiza kufumuliwa kwa Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO ) kufuatia kituo hicho kushindwa kuwahudumia Wananchi kwa viwango vinavyotarajiwa. Ametoa agizo hilo leo tarehe 9 Januari, 2025 jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea kituo hicho pamoja na mambo mengine kufuatilia utekelezaji wa maelekezo yake aliyoyatoa mwezi Aprili, 2024. Dkt. Biteko ameshangazwa na hatua ya TANESCO kuweka kando maelekezo ya mwezi Aprili 2024 yaliyolitaka Shirika hilo kuondokana na matumizi ya namba za kulipia kwenye utoaji wa huduma na kuomba namba ya bure ya huduma (free toll number) kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania -TCRA ili kuwapa unafuu wananchi wanaohitaji huduma za TANESCO. " ...