TLS KULINDA UTAWALA WA SHERIA, KUMSHTAKI MAKONDA TAARIFA KWA UMMA
Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Tundu Lissu, akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana kuhusu maazimio yaliyofikiwa na Baraza la Uongozi la chma hicho na hatua za kuchukus dhidi ys Serikali. Kushoto ni Makamu wa Chama hicho Godwin Ngwilimi na Kulia ni Wakili na Mwenyeji wao Stephine Kuwayawaya. Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) limemaliza kikao chake cha kawaida cha siku mbili kilichofanyika Dodoma kwa kuazimia kuchukua hatua kadhaa zenye lengo la kulinda Utawala wa Sheria na uwajibikaji katika nchi yetu. Akitangaza maazimio ya Baraza hilo, Rais wa TLS na Mwenyekiti wa kikao hicho, Mh. Tundu A.M. Lissu, alizitaja hatua zitakazochukuliwa kuwa ni pamoja na TLS kufungua mashtaka binafsi ya jinai dhidi ya Mkuu wa Dar es Salaam, Paul Makonda aka Daudi Albert Bashite, kwa tuhuma za makosa mbali mbali ya jinai ikiwamo kutumia vyeti feki, ujambazi wa kutumia silaha, matumizi mabaya ya madaraka, n.k. Mh. Lissu alisema: