LOWASSA AKOMBA WAPIGA KURA KUSINI
Mgombea
wa Ubunge anaekubalika na wananchi wa Masasi kupitia Mwamvuli wa Chama cha
Wananchi CUF, Ismail Makombe (Maarufu kwa Jina la Kundambada), akizungumza
machache na wananchi hao waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Boma
Mwenyekiti Mwena wa Ukawa, Dkt. Emmanuel Makaidi akiwa ameambatana na Mkewe, wakiwasalimia wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akizungumza jambo na Mke wa Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Dkt. Emmanuel Makaidi (kulia), Mama Modesta Makaidi, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara, waliofikia kusikiliza sera zake katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma
Lowassa, akiwa haamini umati wa watu waliokuja kumpokea na kuzungumza na kisha kuwaomba kura kwake na kwa madiwani na wabunge wanaounda UKAWA
Sehemu ya Umati wa Wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara wakiwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Boma, leowakimshangilia na kuuponda utafiti wa TWAWEZA
Akizungumza nao
Lowassa kama Yohana mbatizaji hana maneno mengi elimu, elimu elimu bulee mengine atayashughulikia kwa pamoja na wananchi wenyewe
Akiondoka na kuwaaga katika eneo hilo.
Wajibuni Twaweza kwa kura-Lowassa
Mwenyekiti Mwena wa Ukawa, Dkt. Emmanuel Makaidi akiwa ameambatana na Mkewe, wakiwasalimia wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akizungumza jambo na Mke wa Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Dkt. Emmanuel Makaidi (kulia), Mama Modesta Makaidi, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara, waliofikia kusikiliza sera zake katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma
Lowassa, akiwa haamini umati wa watu waliokuja kumpokea na kuzungumza na kisha kuwaomba kura kwake na kwa madiwani na wabunge wanaounda UKAWA
Sehemu ya Umati wa Wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara wakiwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Boma, leowakimshangilia na kuuponda utafiti wa TWAWEZA
Akizungumza nao
Lowassa kama Yohana mbatizaji hana maneno mengi elimu, elimu elimu bulee mengine atayashughulikia kwa pamoja na wananchi wenyewe
Akiondoka na kuwaaga katika eneo hilo.
Wajibuni Twaweza kwa kura-Lowassa
Tuwajibu Twaweza
kwa mafuriko ya kura- Lowassa
MUDA mfupi
baada ya Twaweza kutoa matokeo ya utafiti yaliyoonyesha mgombea uraisi wa CCM ,
Dk John Mafufuli anaongoza, Waziri Mku wa Zamani, Edward Lowassa,
anayepeperusha bendra ya Chadema, aliwataka wananchi kujibu utafi huo kwa kura.
Mgombea huyo
anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alisema yeye anasubiri
mafuriko ya kura Okatoba 25.
Akizungumza
jana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Madeko kwenye
Jimbo la Ndanda wilayani Masasi katika Mkoa wa Mtwara, Lowassa alisema “leo
asubuhi (jana) kuna watu waliotoa matokeo ya kura ya maoni wakasema eti
Magufuli amepata kama asilimiwa 65 mimi 25”
Wananachi “
waongoo”
“Sisi tujipange
tuwajibu kwenye kura. Nangonja kwa hamu mafuriko ya kura, kutoka kwa wana
ndanda Watanzania wote.
Tarehe 25 mnipe
kura, mtashindwa kuona hizi mvi?,” alisema Lowassa huku akiwa navua kofia.
Naye Waziri Mkuu
Mstaafu, Fredrick Sumaye akizungumzia suala hilo, alisema utafiti huo umepikwa
ili kuwahadaa wananchi wajue kwamba Dk magufuli ndiye anayependwa zaidi na
wananchi.
“Leo wametoa
utafiti feki, hewa, uliotengenezwa. Wanasema ati leo kura ikipigwa Magufuli
atapata kura asilimia 65, na Lowassa asilimia 25,” alisema Sumaye
huku baadhi ya wananchi wakijibu “Waongoo.”
Sumaye
aliendelea kusema kuwa, “tumepita mikoa kibao watu kwa maelfu wanakuja na
kutaka mabadilik;o, wao wakija hapa watu hawafiki hata robo ya ninyia, Dk
Magufuli mpaka azoe watu na malori.”
Alisema hakuna
jema lolote mpaka sasa ambalo CCM imefanya, “ leo wanataka kucheza na akili za
watu ili watu wajue kuwa Magufuli ndiye anayependwa.”
Nataka
maendeleo
Akizungumzia
suala la Maendeleo, Lowassa alisema amechoka na umasikini ambao umekuwa
ikiimbwa tangu mwaka 1962.
Alisema atataka
wananchi wawe huru ndani ya nchi yao ili kama ni wakitaka kuuza mazao ya ya
biashara wafanye hivyo sehemu yoyote.
“Na nitaanza na
eneo la elimu, kubadili mfumo wa elimu na maslahi ya elimu yawe bora na kilimo
cha kisasa. Nilivyokuwa Bukoba nilisema kama Kahawa Uganda ni bei nzuri watu
waruhusiwe kuuza huko.
Lazima raia wawe
huru, kama ulikuwa uwasaidii wananchi wakati wakati wanalima kwanini uwaingilie
wakati wa kuuza?,” alisema Lowassa.
Kuhusu suala la
gesi asili, alisema serikali ya Ukawa ikiingia madarakani ahatahakikisha
wanapitia upya mikataba ya gesi na mafuta ili kuona kama inanufaisha wananchi,
haswa wale wa mikoa ya kusini na Watanzania kwa ujumla.
Sumaye: Ule
wako Nape
Sumaye alisema
baada ya kuzungumza mambo mbalimbali ya serikali ameanza kutishwa ikiwa ni
pamoja na Kauli ya Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye aliyemtaka kiongozi huyo
kunyamaza vinginevyo atamshughulikia.
“Anasema Sumaye
anyamaze vinginevyo tutamshukunghulikia, sijui atanishughulikia kwa lipi,
lakini ole wake nikipata tatizo lolote.
Nataka wapande
jukwaani watuambie madawa ya kulenya yanayokamatwa kila siku kwa maguni ni ya
nani na mpaka sasa kafanywa nini?
Meno ya tembo ya
tembo yanayokamatwa huko ni ya nani na mpaka sasa hivi kafanywa nini?
Meli mbovu
iliyopo Dar es Salaam ambayo sasa imeletwa Lindi ili kuwadanganywa wananchi
nani kainunua na kafanywa nini, mabehewa mabovu nani kanunua na kachukulia
hatua gani.
Siyo nikisema
haya unasema utanishughulikia, utanishughulikia we nani?
Kama hawana
majibu ya haya lazima waondoke, ndiyo utaratibu duniani kote, wanashangaa nini?
Kama hawataki
kuondoka wasema kuwa wao ni madkteta tujue.
Kama ni chama
cha siasa kama vingine, Oktoba 25 wanaondoka asubuhi,” alisema Sumaye.
Sumaye
alisema hali ya kutishwa haipo kwake pekee bali hata kwa wananchi ambao
wanadanganywa kuwa wakichagua upinzani nchi itakuwa na vita.
Alisema Libya,
Misri ilipata machafuko baada ya serikali kukataa kusikiliza wananchi.
“Ndiyo hivyo CCM
wanataka kufanya, wakikataa itakuja kutokea hayo, watakaoamua kiti cha urais
kiende wapi ni kura zenu,” alisema Sumaye.
Nguvu ya Umma
na wabunge
Lowassa jana
alilazimika kutumia mahakama ya wananchi kuchagua Mgombea Ubunge wa Jimbo la
Masasi ambapo kulikuwa na msuguano wa Chadema na NLD.
Katika jimbo
hilo, Chadema wamemsimamisha Cecil David Mwambe, huku NLD ikimsimamisha
Angelous Gadriel Thomas.
Kutokana na hali
hiyo, wagombea wote hao walipewa nafasi ya kupanda jukwaani na kila mmoja kwa
wakati wake aelekeze changamoto za jimbo la Ndanda.
Baada ya kunadi
sera zao, Lowassa kabla ya kumaliza kuhutubia aliwaita wagombea hao na kisha
kihoji wananchi ni nani wanayemtaka na uwanja mzima ukamchagua Mwambe.
Lowassa alihoji
wananchi hao mara mbili kisha kumuuliza mgombea na NLD kama anakubaliana na
matokeo.
“Sikubaliani
nayo kwa sababu yalishapangwa,” alisema.
Baada ya kauli
hiyo Lowassa alisema kwa mamlaka aliyopewa anamtangaza mgombea wa Chadema kuwa
mgombea wa jimbo hilo kwa kuwa amekubaliwa na wananchi walio wengi.











Comments
Post a Comment