SIKU YA TAKWIMU AFRIKA YAFANYIKA CHAMWINO JIJINI DODOMA
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Janeth Mayanja (wapili kulia na Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa 9wapili kushoto) wakiwasili katika shule maalum ya Buigiri wanayosomawatoto wenye mahitaji maalum
Leo ni siku ya kimataifa ya takwimu imeadhimishwa, ambapo Tanzania inaungana na nchi nyingine za Kiafrika kuhakikisha inazipa kipaumbele takwimu katika kupanga maendeleo ya wananchi kwenye juhudi za kuelekea kufanikisha maendeleo endelevu.
Hayo yamezungumzwa leo katika eneo la Chamwino jijini Dodoma, amabapo mgebi rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya hiyo Janeth Mayanja pamoja na Mtakwimu Mkuu nchini DKT. Albina Chuwa na pacha wake wa Zanzibar, Salum Kassim Ali
Mtakwimu mkuu wa serikali ya Tanzania Dkt Albina Chuwa ameeleza jinsi ambavyo takwimu ni suala la kila siku la maisha ya kila binadamu.
“Katika kaya kwa mfano, wakati unapanga matumizi na mapato ya kaya yako, lazima ugawanye ujue kwamba ninunue kitu fulani nitatumia kiasi gani cha fedha. Ile ni takwimu tayari. Mapato haya nimeyapata niyagaweyeje, shule,niyafanye huku. Tunasema hizo ni takwimu za mapato na matumizi katika kaya. Kwa hiyo hapo ni kwamba mtu ni lazima kwa kawaida uwe na kitabu chako ambacho unapanga matumizi yako na mapati, halafu mwisho wa mwezi unajipanga vizuri sawasawa na mshahara wako uone kwamba uko katika ile hali unayotaka kuishi. Kwa hiyo ile ni takwimu.”
Dkt .Chuwa ameongeza kuwa hivi sasa Afrika imeazimia kuzipa takwimu kipaumbele katika mipango ya maendeleo
“Tunataka, tumeazimia kuendeleza tasnia ya takwimu Afrika na duniani. Huu utashi wa kisiasa ulioanza katika Umoja wa Mataifa unashuka hivyo. Angalia mawaziri wetu wa fedha na mipango ya Afrika waliazimia kwamba takwimu ikae pale ju na ndio muongozo wa agenda ya Afrika.
Mpango wa maendeleo wa miaka mitano, kwa hiyo unakuta agenda ya takwimu iko mbele. Mi ninavyomsikia Rais wangu anasoma hotuba yake , anatumia takwimu, nasema, ah! Nakushukuru Mungu. Kwasababu sasa takwimu imeingia, siyo suala la zamani watu wanapanga kwa kutumia uzorfu.”
Aidha Mayanja , anasema bila kutumia Takwimu Wilaya hiyo haiwezi kutekeleza mipoango yake lazima ifahamu kila kaya inawatu wangapi mahitaji yao ni yapi na waweze kuwatekelezea mahitaji yao.
Wakati wa Maadhimisho hayo yalieda sambamba na utoaji wa msaada wa vifaa vya ujezi wa jiko la kupikia shule maalum ya Buigiri (blind)ambapa hadi fundi amelipwa fedha yote ya ujenzi.
Mtakwimu wa Zanzibar, Salum Kassim Ali, akizungumza katika maadhimisho hayo
Wasanii wa Mchoya wakitoa burudani katika maadhimisho hayo
Wananchi waliojitokeza katika hafla hiyo
Wanafunzi wa Chuo cha UDOM wakitoa burudani
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Janeth Mayanja, akimkabidhi baadhi ya vifaa ya ujenzi wa jiko Mwalimu Mku wa Shule ya Bwigiri vilivyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu leo
Mtakwimu Mkuu Dkt. Albana Chuwa (kulia), akimkabidhi stakabadhi ya malipo ya fundi wa ujenzi wa jiko Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Janaeth Mayanja
Makabidhiano ya vifaa hivyo yakifanyika leo shuleni hapo
Mkuu wa Wilaya Chamwino Mayanja, akizungumza shuleni hapo
Mtakwimu Mkuu Dkt. Albina Chuwa, akizungumza shuleni hapo kabla ya kukabidhi msaada
Wanafnzu wa shule hiyo wakiwa katika hafla hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Janeth Mayanja, akiukalibisha ugeni wake kutoka Ofisi ya Tawimu walipomtembelea leo asubuhi na kuwa na mazungumzo mafupi
Mtakwimu Mkuu Dkt. Albina Chuwa, akizungumza ofisini kwa Mkuu wa Wilaya baada ya kukalibishwa
Mtakwimu Mkuu Dkt. Albina Chuwa, akizungumza na maofisa wa ofisi yake baada ya kuwasili ofisini kwa mkuu wa Wilaya ya Chamwino jijin Dodoma leo asubuhi
Comments
Post a Comment