MAAJABU YA RAIS SAMIA YAENDELEA KATIKA UTALII ------MCHUMI MASOLWA
Mchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini Daniel Masolwa, amesema Idadi ya watalii walioingia nchini iliongezeka hadi kufikia 1,560,641 kipindi cha januari hadi Septemba 2024, ikilingznishwa na watalii 1,299,994 walioingia nchini katika kipindi kama hicho mwaka 2023 ikiwa ni ongezeko la watalii 260,640 sawa na asilimia 20.0.
Wanahabari wakimsikiliza Mchumi Masolwa alipokuwa akivavadua ukuaji wa uchumi na ongezeko la watalii nchini
Mchumi huyo ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na wanahabri akizungumzia ukuaji wa uchumi nchini , aliendelea kusema kwamba Idadi ya watalii walioingia nchini katika kipindi cha Januari hadi Septemba kuanzia mwaka 2021 hadi 2024, imendelea kuongezeka kutoka 624,396 mwaka 2021 hadi 1,560.641 mwaka 2024. ikiwa ni ongezeko zaidi ya mara mbili nusu ya ilivyokuwa mwaka 2021. kuongezeka kwa idadi kunatokana na hatua mbalimbali za kutangaza utalii husani uliofanywa na Jemedari wetu Mkuu Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na taasisi zake ambapo watalii wa nje na ndani wamekuwa wakiongezeka kila kuchwao.
Wanahabari wakimsikiliza Mchumi Masolwa alipokuwa akivavadua ukuaji wa uchumi na ongezeko la watalii nchini
Comments
Post a Comment