WAGONJWA 19,371 WATIBIWA KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KUTOKA JANUARI HADI MACHI 2018.
Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kipindi cha miezi mitatu ya Januari
hadi Machi 2018 imeona jumla ya wagonjwa 19,371 wenye matatizo
mbalimbali ya moyo kati ya hao wagonjwa wa nje ni 18,481 na waliolazwa
ni 890.
Wagonjwa
105 walifanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua kati ya hao watu
wazima 53 na watoto 52. Kati ya wagonjwa 105 waliofanyiwa upasuaji 66
walifanyiwa na madaktari wetu bingwa wa magonjwa ya moyo watoto wakiwa
ni 35 na watu wazima 31.
Upasuaji
wa moyo wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa
Cathlab ulifanyika kwa wagonjwa 231 kati ya hao watoto ni 20 na wakubwa
211. Kati ya wagonjwa 231 waliotibiwa wagonjwa watu wazima 211
walifanyiwa upasuaji na madaktari wetu wa ndani.
Kwa
kipindi cha miezi mitatu tumekuwa na jumla ya kambi za matibabu nane
(8) ambapo tulifanya matibabu kwa kushirikiana na washirika wetu kutoka
nchi za Ujerumani, Israel, Australia , Marekani, India na Falme za
Kiarabu. Katika kambi hizo jumla ya wagonjwa 39 walifanyiwa upasuaji wa
kufungua kifua kati ya hao watoto 17 na watu wazima 22. Wagonjwa 72
walifanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua kati ya hao watoto 20 na
watu wazima 52.
Tumefanya
upasuaji wa kuunganisha mishipa ya damu (AVF- Arterio Venous Fistula)
kwa ajili ya kusafishia damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo
(Hemodialysis) 36.
Changamoto
kubwa tunayokabiliana nayo ni wagonjwa wengi tunaowapokea mioyo yao
kutokuwa katika hali nzuri hivyo basi tunawaomba wananchi kujenga tabia
ya kupima afya zao mara kwa mara hii itawasaidia kujuwa kama wana
matatizo ya moyo au la na kama wanamatatizo wataweza kupata tiba kwa
wakati.
Wazazi
na walezi tunawaomba wasisahau kupima afya za watoto wao pale
watakapoona kuna hali ya tofauti katika ukuaji wa mtoto kwani magonjwa
mengi ya moyo yanaanzia utotoni. Mtoto akianza kuuguwa magonjwa ya moyo
wazazi wengi wanadhani ni matatizo ya kifua baada ya kumfikisha
Hospitali na kufanyiwa vipimo ndipo inagundulika mtoto anasumbuliwa na
magonjwa ya moyo. Kwa wamama wajawazito wafanye uchunguzi (Fetal
Echocardiography) wa kuangalia kama mtoto aliyeko tumboni anamatatizo ya
moyo.
Aidha
kwa upande wa gharama za matibabu Taasisi yetu imeyagawa katika makundi
manne (4) tuna wagonjwa wanaotibiwa kwa bima mbalimbali ambazo
tumeingia makataba nazo. Wagonjwa wanaolipia gharama zote wenyewe,
wagonjwa wanaochangia kidogo huku gharama zingine zikilipwa na Serikali.
Kundi la mwisho ni wagonjwa ambao hawalipii kabisa gharama za matibabu
ikiwa watakidhi vigezo vyote vya kutokulipa.
Huduma
zetu za matibabu ya moyo zinatolewa kwa watanzania wote wa Bara na
Visiwani. Ifahamike kwamba fedha za matibabu zinazolipwa na wagonjwa
zinatumika kununua vifaa tiba vya moyo kama mlango wa moyo (Valve),
betri ya moyo (Pacemaker) na vinginevyo.
Kutokana
na matibabu ya moyo kuwa ya gharama kubwa tunaendelea kuwasisitiza
wananchi wajiunge na mifuko ya bima za afya ambayo itawasaidia kulipa
gharama za matibabu pindi watakapohitaji kutibiwa. Pia itasaidia
Hospitali yetu kuendelea kujiendesha yenyewe kwa kushirikiana na
Serikali na wadau wengine.
Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
19/04/2018
UJANGILI NCHINI WAPUNGUA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 50 - DK. KIGWANGALLA
Na Hamza Temba-Dodoma
Serikali imefanikiwa kudhibiti vitendo vya ujangili hapa nchini kwa zaidi ya asilimia 50.
Hayo
yameelezwa jana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla wakati akizungumza na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Sarah
Cooke ofisini kwake mjini Dodoma.
Mazungumzo
hayo yalilenga kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kuimarisha ushirikiano
baina ya nchi hizo mbili katika sekta ya uhifadhi na maendeleo ya
utalii.Dk.
Kigwangalla alisema katika kipindi cha miezi sita iliyopita hakuna
mauaji mapya ya wanyamapori yaliyoripotiwa na kwamba nyara zinazokamatwa
hivi sasa ikiwemo meno ya tembo na ngozi za wanyamapori ni masalia ya
zamani.
Amesema
mafanikio hayo yametokana na juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali
kudhibiti vitendo vya ujangili ikiwemo doria za mara kwa mara za
kiitelijensia ambazo zimekuwa zikishirikisha vyombo mbalimbali vya
ulinzi na usalama pamoja na raia wema.
Alisema
Serikali itaendelea kudhibiti vitendo hivyo kwa kuimarisha ulinzi
katika maeneo ya hifadhi nchini ikiwa ni pamoja na kuanzisha jeshi
maalum la usimamizi wa Misitu na Wanyamapori, Sheria ya wanyamapori na
za taasisi za uhifadhi zimeanza kufanyiwa marekebisho kuwezesha
mabadiliko hayo.
Katika
hatua nyingine Dk. Kigwangalla amemueleza balozi Cooke kuwa, Serikali
kupitia Wizara yake inaendelea kuimarisha vivutio vya utalii hapa
nchini kwa kupanua jeografia ya maeneo ya utalii sambamba na kuongeza
vivutio ili kuongeza idadi ya watalii na mapato.
Amesema
Serikali itajenga makumbusho ya Marais Wastaafu wa Tanzania mjini
Dodoma pamoja kuanzisha makumbusho ya meno ya tembo katika miji ya Dar
es Salaam, Arusha, Iringa na Dodoma.
Sambamba
na hayo amesema Serikali itaanzisha mwezi maalum wa maadhimisho ya
urithi wa Mtanzania ambao utafanyika mwezi Septemba kila mwaka pamoja na
kuendeleza utalii wa mikutano.
Amesema
Serikali pia itaanzisha Mamlaka ya Usimamizi na Uendelezaji wa Fukwe
nchini ili kuimarisha utalii wa fukwe pamoja na kutambua barabara
iliyokuwa ikitumika katika biashara ya utumwa wakati wa ukoloni ili
iweze kutumika kiutalii.
Akizungumzia
migogoro ya mipaka iliyopo baina ya wananchi na maeneo ya hifadhi, Dk.
Kigwangalla alisema Serikali itatatua migogoro hiyo kwa kushirikisha
wananchi sambamba na kuwasaidia kutatua changamoto za msingi ambazo ni
kuimarisha maeneo ya malisho ya mifugo, upatikanaji wa maji kwa ajili ya
wananchi na mifugo, mpango bora wa matumizi ya ardhi na uendelezaji wa
kilimo na ufugaji.
Kwa
upande wake balozi Cooke alisema nchi yake itaendelea kuimarisha
ushirikiano inaoutoa kwa Serikali ya Tanzania katika kudhibiti mtandao
wa uhalifu wa madawa ya kulevya, rushwa na ujangili.
Alisema
kwa sasa watalii zaidi ya 75,000 wa Uingereza hutembelea Tanzania kila
mwaka na wengine wamewekeza katika sekta utalii hapa nchini, hivyo
akaiomba Serikali kurekebisha baadhi ya changamoto chache zilizopo
katika sekta hiyo kwenye mtiririko wa kodi.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na balozi wa
Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma jana
ambapo walijadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano katika
sekta ya uhifadhi na maendeleo ya utalii.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla.
Balozi wa Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiaga na balozi wa
Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma jana baada
ya mazungumzo yaliyolenga walijadili mambo mbalimbali ya kuimarisha
ushirikiano katika sekta ya uhifadhi na maendeleo ya utalii.
Wednesday, April 18, 2018
Wadau wa dawa na vifaa tiba nchini watakiwa kuchangamkia fursa
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Josephat Kandege amewataka wauzaji,
waagizaji, wasambazaji na wadau wote wa dawa pamoja na Vifaa Tiba Nchini
kuchangamkia fursa inayotolewa na Serikali ya kuwa Mshitiri mteule
‘Prime Vendor’ kusaidia katika utoaji wa dawa katika Mikoa yote
Tanzania.
Kandege
ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha Wadau wa dawa ‘Vendors
Forum’ kilichoandaliwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na
wadau wa Afya ‘HPSS’ chenye lengo la kuweka uelewa wa pamoja kuhusu
uanzishwaji na utekelezaji wa mfumo wa Mshitiri.
Amesema
“mfumo huu utatumika kupata mahitaji ya bidhaa za Afya pale ambapo
vituo vya kutolea huduma za Afya vya Umma vitakosa au kupata kiwango
pungufu toka Bohari Kuu ya Dawa na pia utasaidia kupunguza kero za Afya
ikiwemo uhaba wa upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za
Afya”.
Sasa
basi ninyi kama wazabuni muhimu katika sekta hii ya Afya wenye Uzalendo
na nia njema na Nchi ya Tanzania mnatakiwa kujitokeza katika mchakato
wa kumpata Mshitiri (Prime Vendor) wa kila Mkoa ambaye atakidhi vigezo
kwa mujibu wa taratibu manunuzi alisema Mhe. Kandege.
Wakati
huo huo Naibu Waziri Kandege aliwafahamisha wadau wa dawa kuwa Serikali
imagatua mipango na bajeti kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya na
inapeleka Fedha moja kwa moja kwenye akaunti za benki zilizofunguliwa
katika kila kituo hii itasaidia katika kufanya manunuzi ya dawa hizo na
kurahisha mchakato wa malipo.
“Hivyo
niwahakikishie kuwa utaratibu wa malipo utakua ni rahisi na wa haraka
zaidi kwa kuwa Hospital, Vituo vya Afya na Zahanati husika zitahusika
kuagiza dawa kwa Mshitiri pale mahitaji ya dawa hizo zitakapokosekana
kutoka MSD” alisema Mhe. Kandege.
Alimalizia
kwa kuwataka Wadau wote wa Dawa kutumia kikao hiki kuelewa kwa undani
kuhusu utaratibu huu na kujitokeza kwa wingi katika mchakato wa kumpata
Mshitiri Mteule kwani zoezi hili litaendeshwa kwa uwazi na kwa usindani
mkubwa.
Mkurugenzi
wa Afya Ofisi ya Rais Tamisemi Dr. Ntuli Kapologwe amesema hivi sasa
wako katika uwekezaji Mkubwa katika Sekta ya Afya kwa kuzingatia kuwa
Bajeti ya Dawa imeongezwa kutoka Bil 31 kwa mwaka 2015/16 hadi kufikia
Bil 269 kwa mwaka 2017/18 hivyo ongezeko hili la bajeti linatakiwa
kwenda sambamba na uhakika wa upatikanaji wa dawa na zenye ubora chini
ya usimamizi makini wa wataalamu wa Afya.
Dr.
Ntuli alisema mpango huu utaleta manufaa kwa wananchi wote ambao
watakua chini ya mpango wa Tele kwa Tele na wale wanaopata huduma
kupitia mfuko wa Bima ya Afya iliyoboreshwa; Tunataka kila mmoja apate
dawa anayoihitaji kwa wakati.
Naye
Mfamasia toka Ofisi ya Rais Tamisemi Regina Richard alisema mfumo wa
Mshitiri Mteule umeanzishwa kwa sababu ya changamoto zilizoonekana awali
za kutumia mzabuni kama vile taratibu za manunuzi kuchukua muda mrefu
na gharama za manunuzi kuwa kubwa na zinazotofautiana kati ya
Halmashauri moja na nyingine ndani ya Mkoa mmoja.
Changamoto
zingine alizozibainisha ni kubadilika kwa bei mara kwa mara kila
manunuzi yanapofanyika, kutokuwa na uhakika wa ubora wa bidhaa kutokana
na kuhifadhiwa na kusafirishwa katika mazingira mbayo si salama na zaidi
baadhi ya wazabuni na watumishi kutokuwa waaminifu.
Matumizi
ya mfumo huu umeelekezwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi, Sera ya
Afya ya Taifa ya mwaka 2007, Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya na Sera ya
Mashirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi.
Kikao
hiki cha wadau wa dawa ‘Vendor Forum’ kimefanyika kwa mara ya kwanza na
kimehusisha wadau kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.
Naibu
Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege(mbele) akifungua
kikao cha wadau wa Afya ‘Vendor Forum’ kilichofanyika katika Ukumbi wa
Dodoma Hotel.
Mkurugenzi
wa Afya Ofisi ya Rais Tamisemi Dr. Ntuli Kapologwe akitoa maelezo ya
awali kabla hajamkaribisha mgeni rasmi kufungua kikao cha wadau wa Afya
Vendor Forum.
Mfamasia Mwandamizi toka
Ofisi ya Rais Tamisemi Regina Richard akielezea malengo la kikao cha
Wadau wa Dawa ‘Vendor Forum’ kilichofanyika katika ukumbi wa Dodoma
Hotel mapema leo.
Wataalam toka Idara ya Afya Ofisi ya Rais-TAMISEMI pamoja na wadau wa Dawa wakiwa katika kikao maalum cha wadau wa dawa.
Naibu
Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege(mbele katikati)
katika picha ya pamoja na baadhi ya wataalamu na wadau wa dawa.

CCM DAR YASHAURI WALIOZIBA NJIA ZA MAJI WAONDOLEWE, YATOA POLE KWA WALIOPOTEZA NDUGU KWASABABU YA MVUA
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
CHAMA
Cha Mapinduzi(CCM), Mkoa wa Dar es Salaam kimetoa pole kwa familia
ambazo zimepoteza ndugu zao kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha huku
kikitoa ushauri kwa Serikali kuwaondoa waliojenga kwenye njia za maji
kwa lengo la kupunguza maafa.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Cylivia Katekamba amewaambia leo waandishi
wa habari kuwa chama hicho kinatoa pole kwa wote ambao wamefikwa na
maafa na kuomba wenye uwezo wa kusaidia walioathrika na mvua hizo
kujitokeza kusaidia.
" Mkoa
wa Dar es Salaam umekumbwa na mafuriko na kusababisha baadhi ya
wananchi kupoteza maisha.CCM mkoa tunatoa pole kwa ndugu, jamaa na
marafiki kutokana na kuondokewa na ndugu zetu kutokana na mvua.
"Tunafahamu
matatizo ya mafuriko yametokea kwetu na hata maeneo mengine duniani
nayo wakati mwingine hukumbwa na mafuriko.Kubwa ni kuendelea kushikamana
na kusaidia kwenye kipindi hiki.CCM tunatoa pole,"amesema Katekamba.
Pia
ametoa mwito kwa walio maeneo hatarishi ni vema wakaondoka maeneo hayo
na kufafanua kutokana kuzibwa kwa mitaro na njia za maji imesababisha
hata maeneo ambayo huwa hayapati mafuriko safari hii maji yamejaa.
Amefafanua
yapo maeneo ambayo watu wamejenga lakini kiuhalisia ni maeneo ambayo
yapo kwa ajili ya kupitisha maji na matokeo yake yanakosa pakupita na
kwenda kwenye makazi ya watu na kusababisha maafa.
Ameshauri
watu wa mipango miji kuangalia namna ya kuondoa changamoto hiyo na
kuongeza kamati ya siasa ya Mkoa wa Dar es Salaam jana usiku imekutana
kujadili hali ya mafuriko."Moja
ya jambo tulilokubaliana maeneo ambayo yanatakiwa kubaki wazi ili maji
yapite lazima mipango miji kuangalia namna ya kufanya,"amesema na
kuongeza ni vema wananchi wa wakazingatia utunzaji wa mazingira kwa
kutoziba njia za maji na kutokata miti ovyo.
Alipoulizwa
kuhusu waliojenga kwenye njia za maji, Katekamba amejibu kuwa kazi ya
Chama ni kuisimamia Serikali na hivyo moja ya jambo ambalo wanataka
kuona linafanyika ni kuwaondoa waliojenga maeneo hayo.
Pia
ameomba wananchi kuibua na kuwabainisha watu ambao wamejenga kwenye
mifereji ya kupitisha maji badala ya kukaa kimya huku akielezea CCM Mkoa
wa Dar es Salaam walikuwa na sherehe yao ya familia ya Wana-CCM Aprili
21 mwaka huu ambayo Mwenyekiti wake ni Idd Azan lakini wameiahirisha
kutokana na mafuriko ya mvua na athari zilizotokea.
Hata
hivyo, Katekamba pamoja na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali ya mkoa
wamefanya ziara ya kukagua mitaa iliyokumbwa na mafuriko na kuona hali
halisi.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dar es Salaam Cylivia Katekamba(wa
kwanza kushoto) akizungumza ma waandishi wa habari leo jijini wakati
anatoa pole kwa waliokumbwa na mafuriko na familia ambazo zimepoteza
wapendwa wao kwasababu ya mvua zinazonyesha.
Watanzania wahimizwa kujenga utamadunI wa kujisomea vitabu
Watanzania
wamehimizwa kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu kwa ajiri ya kuibua
fursa mbalimbali za kimaendeleo na kuacha tabia ya kutumia vitabu kama
sehemu salama ya kuhifadhia fedha , kama ilivyo kwa baadhi ya watu
maeneo ya vijijin na mjini huku waandishi wa vitabu wakitakiwa
kuendelea kuandika vitabu kwa lengo la kujenga Taifa lenye wasomi.
Hayo
yamesemwa na mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Prof, Ganka Nyamusogoro
wakati wa uzinduzi wa siku ya kusoma vitabu duniani katika chuo kikuu
cha Mzumbe mkoani Morogoro, ambapo amesema jamii nyingi za kitanzania
zimejenga tabia ya kutosoma vitabu kama njia ya kuibua fursa na
kuongeza maarifa baadala yake wanatumia vitabu kama sehemu ya
kuhifadhia fedha jambo ambalo ni kinyume na na malengo ya waandishi wa
vitabu.
Makamu
mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Prof,Ganka Nyamusogoro akikata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa siku ya kusoma vitabu Duniani katika chuo
kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.
Makamu
mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe prof,Ganka Nyamusogoro akikagua moja ya
vitabu vilivyooneshwa na chuo cha mzumbe wakati wa maadhimisho ya siku
ya kusoma vitabu Duniani,ambapo chuo cha mzumbe kimetoa nafasi kwa watu
mbalimbali kusoma vitabu katika eneo hilo ambalo lipo maalumu kwa siku
tatu chuoni hapo kuadhimisha siku hiyo ya kusoma vitabu.
Wanafunzi
wa chuo kikuu cha mzumbe mkoani Morogoro na shule ya sekondari Mzumbe
wakifuatilia kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi katika maadhimisho ya
siku ya kusoma vitabu duniani ambaye pia ni makamu mkuu wa chuo hicho
Prof, Ganka Nyamusongoro hayupo pichani.
Diwani
wa kata ya Mzumbe mkoani Morogoro Recho Kungi wa kwanza
kushoto akisisitizia wanafunzi juu ya umuhimu wa kusoma vitabu katika
maadhimisho ya siku ya kusoma vitabu duniani yaliyo fanyika chuo kikuu
cha Mzumbe mkoani Morogoro.
Makamu
mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Prof,Ganka Nyamusogoro ambaye pia ni
Mgeni rasimi katika maadhimisho ya siku ya kusoma vitabu duniani chuo
kikuu Mzumbe Mkoani Morogoro akisoma vitabu vya tafiti vilivyofanywa
na wanazuoni wa chuo kikuu cha mzumbe mara baada ya kuzindua hafla hiyo.
Mwanafunzi
wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Mzumbe mkoani Morogoro
Alfred Joseph King akijisomea jarida wakati wa maadhimisho ya siku ya
kusoma vitabu duniani, jarida hilo limechapishwa na chuo kikuu cha
Mzumbe mkoani Morogoro.
Makamu
mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Prof,Ganka Nyamusogoro (katikati)
akiangalia hotuba inayohusu maadhimisho ya siku ya vitabu duniani
ambapo kushoto kwake ni mkuu wa idara ya huduma za wasomaji chuo kikuu
cha mzumbe Sarah Mwambalaswa na kulia ni Mkurugenzi maktaba na huduma za
kiufundi chuo kikuu mzumbe Dk Arobogasti Musabila .
Wa
kwanza kushoto ni David Onyango mkutubi wa maktaba ya chuo kikuu cha
mzumbe akimuonesha vitabu vilivyo pangwa katika maktaba maalumu ya
madhimisho ya siku ya kusoma vitabu duniani,wa pili kushoto Makamu mkuu
wa chuo kikuu cha Mzumbe Prof,Ganka Nyamusogoro anae fatia ni Diwani wa
kata ya Mzumbe mkaoni Morogoro Recho Kungi wa mwisho ni mkurugenzi
maktaba na huduma za kiufundi chuo kikuu mzumbe Dk Arobogasti Musabila
TAMASHA LA AMKA KIJANA, TUIJENGE IRINGA YETU LAFANA MJINI IRINGA
Mkuu
wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela (kushoto) akifurahia burudani
iliyokuwa ikitolewa na msanii wa Muziki wa Singeli, Dulla Makabila
wakati wa Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu lililofanyika
uwanja wa MwembeTogwa, Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda nae hakuwa nyuma kutoa burudani.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akizungumza na
wana-Iringa waliojitokeza katika amasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa
Yetu lililofanyika uwanja wa MwembeTogwa, Iringa mwishoni mwa wiki
iliyopita.
Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza, Msanii wa Bongo Movies, Steve Nyerere
ambao ndiyo waandaaji wa Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu
akizungumza machache na wakazi wa Iringa juu ya kutunza Amani, Upendo na
Mshikamano wetu katika uwanja wa MwembeTogwa, Iringa mwishoni mwa wiki
iliyopita.
Mkuu
wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiwatambulisha wasanii wa
Bongo Movie waliofika katika Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa
Yetu lililofanyika uwanja wa MwembeTogwa, Iringa mwishoni mwa wiki
iliyopita.
Mratibu wa Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu, Msanii wa Bongo
movies, Single Mtambalike (Rich Rich) akizungumza machache wakati wa
tamasha hilo lililofanyika uwanja wa MwembeTogwa, Iringa mwishoni mwa
wiki iliyopita.
Msanii maarufu wa Bongo Movies Jacob Steven 'JB ' akieleza machache.
Msanii maarufu wa Bongo Movies Jacob Steven 'JB ' akimtambulisha msanii mwenzake Weru Sengo.
Msanii wa Kundi la Ze Komed akitoa burudani.
Mchekeshaji maarufu, Mama Asha Boko akitoa burudani.
Dj Choka nae alipata wasaa wa kutoa neno kwa wana-Iringa.
Msanii wa Bongo Movies, Anti Ezekiel akiwasalimu wakazi wa Iringa.
Wanamuziki wa bendi ya Fm Academia Wazee wa Ngwasuma wakitoa burudani.
Wasanii wa Bongo movies wakipata picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza na viongozi wengine wa Mkoa mara baada ya kumalizika kwa Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu.
Comments
Post a Comment