WANAODAI KUONEWA KUHUSU VYETI FEKI WATHIBITISHE

Wabunge wakiwasili leo asubuhi kwa ajili ya kikao cha bunge

 Katibu Mkuu wizaranya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki  Ulusubisya akisalimiana na wajawzito waaliofika bungeni kusikiliza bajeti ya wizara hiyo jana. Picha na Deus Mhagale

 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dk. Laurean Ndumbaro,akizungumza na waandishi wa habari mjini Ddodoma jana kuhusu watumishi waliopatikana na vyeti feki na ajlira ilizotoe serekalini. Kulia ni Mkurugenzi wa Uendelezaji Sera Mathias Kabunduguru. Picha na Deus Mhagale




SERIKALI, imesema watumishi wa umma walioorodheshwa kwenye orodha ya watumishi wa umma wenye vyeti feki, wakati hawakutakiwa kuwekwa, wakate rufaa.
  • Kauli hiyo, imetolewa leo  na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk. Laurean Ndumbaro, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
“Kama mtakumbuka, uhakiki wa vyeti feki kwa watumishi wa umma, ulihusisha vyeti vya kidato cha nne, kidato cha sita, ualimu na taaluma zingine.
“Baada ya uhakiki huo, iliagizwa watumishi 9,932 waliokuwa na vyeti feki, waondolewe katika ajira, watumishi 1,538 wenye vyeti vyenye utata kwa maana kwamba vinatumiwa na watu zaidi ya mmoja, wathibitishe vyeti vyao kabla ya Mei 15 mwaka huu na mishahara yao isimamishwe hadi uhakiki utakapokamilika.
“Wale watumishi 11,596 waliogundulika kuwa na vyeti pungufu, wanatakiwa kuwasilisha vyeti vyao vikaguliwe kabla ya Mei 15 mwaka huu, vinginevyo watachukuliwa hatua.
“Lakini, wale wanaodai kwamba wamewekwa kwenye orodha ya wenye vyeti feki wakati hawakutakiwa kuwa huko, tunawaomba waandike barua za kukata rufaa kwa Katibu Mkuu Utumishi kupitia kwa waajili wao.
“Waajiri hao, watatakiwa kuwasilisha vyeti hivyo Baraza la Mitihani la Taifa kwa ajili ya uhakiki zaidi kabla ya Mei 15 mwaka huu.
“Pamoja na hayo, ieleweke kwamba, baadhi ya watumishi wakati wanaajiriwa, waliwasilisha vyeti vya matokeo mengine ya sekondari na wakati wa uhakiki, walionyesha vyeti vingine.
“Lakini, naomba ieleweke kwamba, hakuna mtumishi wa umma mwenye cheti halali atakayeondolewa katika utumishi wa umma.
“Kuhusu suala la mafao ya watumishi hao, hilo tunaliangalia namna ya kulifanya kwa sababu kuna sheria zinazolisimamia,”alisema Dk. Ndumbaro.
Wakati huo huo, Dk. Ndumbaro alisema wakuu wa idara ambazo huduma zake zimeathiriwa na zoezi la vyeti feki baada ya watumishi kuacha kazi, wanatakiwa kuandika barua kwake ili zitangazwe nafasi za ajira za dharura kwa lengo la kuziba mapengo hayo.
Akizungumzia wizara ambazo taarifa za uhakiki wake hazikutolewa hivi karibuni, alisema zitatolewa Mei 10 mwaka huu baada ya uhakiki wake kukamilika.
Katika hatua nyingine, Dk. Ndumbaro alisema Serikali itaajiri watumishi 1,500 kuanzia sasa hadi mwisho wa Bunge la Bajeti linaloendelea mjini hapa.
Kwa mujibu wa Dk. Ndumbaro, ajira hizo zimetolewa ili kukabiliana na uhaba wa watumishi wa umma ulioko katika sekta mbalimbali serikalini.
“Katika hili, waajiri watatakiwa kuhakiki vyeti vya waombaji wote kabla hawajaajiriwa ili kuepuka uwepo wa watumishi wengine wenye vyeti feki,” aliagiza.
Wakati Dk. Ndumbaro akisema hayo, awali Mbunge wa Viti Maalum, Rhoda Kunchele (Chadema), aliliambia Bunge, kwamba watumishi wanne wa umma wamelazwa mkoani Katavi, baada ya majina yao kuonekana katika orodha ya watumishi wenye vyeti feki.
Kutokana na hali hiyo, alitaka Serikali iliangalia suala hilo kwa kina kwa kuwa baadhi ya watumishi waliowekwa katika orodha hiyo, wanadaiwa kuwa na elimu ya sekondari wakati hawajawahi kusoma kusoma huko.
Hivi karibuni, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki, alimkabidhi Rais Dk. John Magufuli, orodha ya watumishi wa umma wenye vyeti feki.
Hata hivyo, Kairuki alisema katika uhakiki wao, hawakuhusisha wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wabunge na wanasiasa wengine.

Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.