WANATAALUMA WAMUAGA MAREHEMU PROFESA SAMWEL MASELE ALIYEWAHI KUWA MKURUGENZI MKUU HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI
Mwili
wa aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili
ukiwasili katika kiwanja cha Graduation Square MUHAS ukisindikizwa na
wanataaluma jana April 11, 2017 ambapo mazishi yamefanyika katika
makaburi ya Kinondoni leo April 12, 2017 Jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru (kulia)
akiangalia mwili wa Marehemu Profesa Maselle ukishushwa toka katika
gari maalumu lililokuwa limebeba mwili huo jana, wapili kulia ni Profesa
Ayubu Magimba
Mwili
wa aliyewahikuwa Mkurugenzi Hospitali ya Taifa Muhimbili Ukiwasili
katika kiwanja cha Graduation SQuare Muhas ambapo taratibu za kutowa
heshima za mwisho zilifanyika jana April 11, 2017 na leo April 12, 2017
mwili huo unatarajiwa kupumzishwa katika makaburi ya Kinondoni Jijini
Dar es Salaam
Wanataaluma
mbalimbali wakiwa wanaushusha mwili wa mpendwa wao marehemu Profesa,
Samuel Maselle kwa maandalizi ya kutowa heshima za mwisho jana
Baadhi
ya viongozi katika meza Kuu akiwemo Profesa, Ephata Kaaya (wa tatu
kushoto) wapilikushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili Profesa, Lawrence Museru na wa kwanza kushoto ni Profesa Ayub Magimba
Baadhi ya wanafamilia na wana Taaluma wa Muhas
Kaimu Mkuu wa Skuli ya Tiba, (MUHAS) Dokt, Erasto Mbugi akisoma wasifu wa Marehemu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence
Museru akisoma wasifu kwa niaba ya Hospitali ya Taifa na kutowa
Rambirambi kwa niaba ya wafanyakazi wa hospitali hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete akisoma wasifu wa Marehemu Maselle kwa niaba ya Taasisi hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa, Muhimbili (MOI) Dokt,
Respicious Boniface akisoma wasifu kwa niaba ya Taasisi hiyo na kutowa
Rambirambi kwa niaba ya wafanyakazi wake
Ndugu
wa Marehemu akishukuru kwa wote waliyojitolea kwa hali na mali
kushirikiana na familia bega kwa bega kusaidia kuokoa maisha ya ndugu
yao na hata mlipo sikia ndugu yetu katutoka hamkutuacha peke yetu na
mmekuwa mstari wa mbele kufanikisha shughuli nzima za maandalizi ya
kumsindikiza mpendwa wetu Profesa Maselle kuelelea katika nyumba yake ya
milele na mmekuwa nasi mwanzo hadi kufikia tulipo fikia. nawashukuruni
sana na mungu awabariki
Sehemu ya wanataaluma mbalimbali
Baadhi ya wana taaluma wakifatilia kwa umakini yaliyokuwa yakiendelea Chuoni hapo
Aliyewahi
kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dr. Marina
Njelekela akitowa heshima za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa
aliyewahi kuwa Mkurungezi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili
Profesa, Samuel Maselle katika kiwanja cha Graduation SQuare Muhas
Waombolezaji wakitowa heshima za mwisho
Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa (aliyeshika mwamvuli) akitowa heshima za mwisho katika jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Hospitali hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa, Muhimbili (MOI) Dokt, Respicious Boniface akitowa heshima za mwisho katika jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Hospitaliya Taifa Muhimbili
Wanataaluma
wakiubeba mwili wa marehemu Maselle kuuweka katika gari maalumu tayari
kwa kuelekea nyumbani kwa marehemu Mbezi Beach
Mwili wa Marehemu Maselle ukiingizwa jana katika Gari
LAPF WATAMBULISHA HUDUMA YA UWEKAJI AKIBA KWA WANACHAMA WA HIARI
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Bw. Ramadhani Mkeyenge
akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu dhana nzima ya utaratibu wa uwekaji
akiba kwa hiari kwenye Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwenye mkutano uliofanyika
Makao makuu ya Mfuko mjini Dodoma .
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw.
James Mlowe akizungumza na waandishi wa Habari mjini Dodoma kuhusu umuhimu
wa matumizi ya teknolojia ikiwemo huduma za M-pesa na Tigo-pesa katika kuwafikia
Watanzania walio wengi ili wajiunge na kuweka akiba kupitia “LAPF Jiongeze Scheme”.
Meneja mwenye dhamana na Skimu ya uchangiaji wa hiari (LAPF Jiongeze Scheme)
Bi. Hanim Babiker akizungumzia taratibu mbalimbali zinazotakiwa kufuatwa ili kuweka
akiba kwa njia ya M-pesa na Tigo-pesa wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari
mjini Dodoma.
Afisa huduma kwa wanachama wanaoweka akiba kwa hiari (LAPF Jiongeze Scheme)
Bw. Juma Venerando akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari jinsi Mfuko wa
Pensheni wa LAPF ulivyojipanga kuendelea kuboresha zaidi huduma kwa wanachama.
Mwakilishi wa Kampuni ya Tigo Mkoani Dodoma Bw. Gideon Morris akizungumza na
waandishi wa Habari jinsi kampuni hiyo ilivyojipanga kiteknolojia katika kuhakikisha
ubora zaidi wa huduma zao za Tigo-pesa na hivyo kuwawezesha watanzania wote
kuweka akiba ya hiari Kwenye Mfuko wa LAPF.
Mwakilishi wa Kampuni ya Vodacom Mkoani Dodoma Bw. Balikulije Mchome
akizungumza na waandishi wa Habari jinsi kampuni hiyo ilivyojipanga kiteknolojia katika
kuhakikisha ubora zaidi wa huduma zao za M-pesa na hivyo kuwawezesha watanzania
wote kuweka akiba ya hiari katika Mfuko wa Pensheni wa LAPF.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia kwa makini maelezo
mbalimbali yaliyotolewa kwenye utambulisho wa huduma za uwekaji wa akiba ya hiari
kwa njia ya M-pesa na Tigo-pesa kwenye Mfuko wa Pensheni wa LAPF, mkutano
uliofanyika mjini Dodoma.
RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA RELI YA KISASA STANDARD GAUGE KUTOKA DAR HADI MOROGORO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na Mkewe Mama
Janeth Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ujenzi wa
Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam
hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi mikoa ya
Kigoma na Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiweka jiwe la msingi
Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es
Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi
Kigoma na Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia majina ya baadhi ya
wataalamu mbalimbali waliohusika katika mchakato wa Ujenzi huo
wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es
Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi
Kigoma na Mwanza. Wakwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO)
Masanja Kadogosa akiwa ameshika majina hayo.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akichota
mchanga na kuweka kama ishara ya kushiriki katika ujenzi huo wa
Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam
hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na
Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiangalia kibao cha jiwe la msingi cha
Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es
Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi
Kigoma na Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa, Mama Janeth Magufuli
wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO Masanja
Kadogosa wakati akielezea kuhusu ujenzi wa Reli ya Kisasa
Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani
Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa amechuchumaa kwenye mfano wa
Reli ya Kisasa (SGR) na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa, Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa RAHCO Masanja Kadogosa, Mwenyekiti wa Kamati
ya Kudumu ya Miundombinu Profesa Norman Sigala mara baada
ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Reli hiyo, wengine katika
picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli pamoja na Hawa
Ghasia (Mb).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa wakati akipita katika
katika ya mfano wa Reli hiyo itakayojengwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi
waliohudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi Ujenzi wa Reli
ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi
mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza.
Mfano wa Reli hiyo ya Kisasa ya Standard
Gauge SGR itakayojengwa kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro
na baadae kuendelea hadi mikoa ya Mwanza na Kigoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kaimu Mtendaji Mkuu
wa RAHCO Masanja Kadogosa wakati akielekea kuweka jiwe la
Msingi ujenzi wa Reli hiyo ya Kisasa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya kuweka jiwe la Msingi
ujenzi wa Reli hiyo ya Kisasa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mufti Mkuu wa
Tanzania Shekhe Abubakary Zubeiry mara baada ya kuweka jiwe
la Msingi katika eneo la Pugu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza msanii Mrisho Mpoto
mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi huo wa Reli ya
Kisasa Pugu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.
Comments
Post a Comment