JUKWAA LA KATIBA NA KATIBA MPYA
Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwa hilo Hebron Mwakagenda,akizungumza mwanzoni mwawiki hii na wanahabari akiitaka Serikali ikamilishe mchakato wa katiba mpya iziangatie matakwa ya Watanzania na uhalisia wa mmchakato wenyewe
Nchi yoyote
Duniani inayoongozwa kwa mujibu wa sheria ni lazima iwe na katiba yake ambayo
itakuwa inamuongoza kila mtu au kiongozi anapotaka kufanya maamuzi yake
yasiyokuwa ya kidikiteta hapo wanananchi watakuwa na imani nae .
Nchini
Tanzania tulikuwa na katiba ambayo wengi walidai imepitwa na wakati na utawala wa awamu ya nne ukatoa mamilioni
ya fedha kutafuta maoni kwa ajili ya katiba mpya.
Kilichofanya
watanzania wasipate katiba mpya inadawa
kujaza makada wengi wa chama cha mapinduzi CCM kwenye Bunge la kuipitisha
katiba hiyo, matokeo yake ikashindikana
sasa tumekuwa taifa la ajabu fedha zimeliwa na katiba haipo
iliyotalajiwa.
Jukwaa la
Katiba limekuwa kisemeo la Watanzania wasiokuwa na kipaza sauti cha kusikika
wanadai mwendelezo wa katiba yao ulioshindikana kipindi kile uendelee ili
waondokane na katiba iliyojaa viraka.
Sheikh Juma
Ali Maneno, akizungumza na mwandishi wa makala hii, aliwapongeza viongozi wa
Jukwaa la Katiba kwa moyo wao wa kuendelea mazungumzo ya kuataka viongozi wa nchi hii wamuogope mungu ili wawaletee wananchi katiba yao ambayo itakuwa dira
kwao waondokana na mambo ya kubahatisha na kutishwa na baadhi ya viongozi wenye
kutaka kuambudiwa hata kama uwezo wa kiutendaji hawana.
Na hivi sasa hata vyombo vyahabari vimeanza
kuandamwa kuacha kuwafuata fuata wakubwa pindi wanapotekeleza mambo yao hata kama kwawanananchi na vyombo vya habari wanaona hayafai
Historia ya vyombo vya
habari baada ya Tanganyika kupata uhuru wake mwaka 1961 tunaelezwa kwamba Serikali ya Tanganyika
ilianza kujipanga kwa kuchukua hatua kadhaa kuhakikisha inarejesha heshima ya wananchi
wake waliokuwa wameonewa, wamenyonywa na kupuuzwa kwa miaka mingi ya utumwa wa
ukoloni.
Katika mikakati hiyo
mnamo mwaka 1967 Serikali ilikuwa chini
ya Chama TANU ilianzisha kile
ilichokiita Azimio la Arusha ikiwa na
lengo la kuhakikisha njia zote za uchumi zinamilikiwa na umma kabla ya mwaka 1970 aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Hayati Mwalimu Julius Nyerere kutoa sera mpya ya vyombo vya habari kupitia gazeti
la The Standard (ambalo kwa sasa linaitwa Daily News.
Katika sera hiyo
ya vyombo vya habari ilivielekeza vyombo vya habari nchini kuunga mkono falsafa
ya Ujamaa na Kujitegemea na dhima kuu ikiwa na mambo matano.
Mambo hayo ni kama ifuatavyo (i) Kuhabarisha wananchi
kuhusu masuala yote muhimu ya ndani na nje ya nchi (ii) Kuelimisha, kufunza
(iii) Kuwa kiungo cha mawasiliano ya serikali kwa wananchi (iv) Kuhamasisha
wananchi katika masuala mbalimbali kama vile ukombozi wa majirani zetu
waliokuwa chini ya ukoloni (v) Kukosoa kwa uhuru vitendo vyovyote vya viongozi
wa chama au serikali ambavyo vinavyoenda kinyume cha misingi au maslahi ya nchi
na kuburudisha.
Hata hivyo pamoja na
sera hiyo kwa upande mmoja kuonekana kuwa ni nzuri, lakini ukiichunguza kwa
upande wa pili wa shilingi, baada ya uhuru Serikali iliendelea kubaki na sheria zile
zile za wakoloni za kudhibiti vyombo vya habari.
Moja ya sheria hizo ni
ile ya magazeti ya mwaka 1976 au ile ya Shirika la Habari Tanzania (SHIHATA) ya mwaka 1976 ambazo
zote kwa pamoja zililenga kudhibiti
mfumo wa habari kwa namna ile ile wakoloni walivyokuwa wanafanya, japo kwa mitazamo
tofauti.
Na hata Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haikuwa na vifungu vilivyotambua au kulinda
dhima ya vyombo vya habari katika jamii. Aidha, hata mwaka 1984 pale vifungu
vya haki za binadamu vilipoingizwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania ya mwaka 1977 bado vyombo vya habari havikutamkwa popote mbali tu na
Ibara ya 18, kifungu cha (i) ambacho kilizungumzia haki ya kila mtu kuwa na
maoni yake, ikiwa ni pamoja na uhuru wa kukusanya, kupokea na kusambaza taarifa
kupitia chombo chochote cha habari bila kujali mipaka na kifungu cha (ii)
kilichosema: kila mtu anayo haki ya kuhabarishwa kuhusu masuala muhimu kwa
maisha yake yanayotokea ndani na nje ya nchi.
Vyombo vya habari kwa
ujumla wake vilidhibitiwa na sera na sheria za vyombo vya habari, lakini pia
mfumo uliojengwa katika falsafa ya Ujamaa na Kujitegemea na uliozingatia tunu
za usawa, utu, umoja na uzalendo.
Vyombo vya habari
vilichukuliwa zaidi kama taasisi za kutoa huduma na si biashara ya kutafuta
faida kama ilivyo leo. Aidha umiliki wa vyombo vya habari ulikuwa ama chini ya
serikali au taasisi.
Watu binafsi
hawakuhamasika kuanzisha vyombo vya habari katika mazingira yaliyokuwapo.
Falsafa ya sekta ya habari na mawasiliano ilikuwa: Mawasiliano kwa ajili ya
maendeleo.
Hali hiyo ndiyo ipo
hadi sasa kutokana na kwamba Ibara hiyo ya 18 ya Katiba inaendelea kueleza kwamba “bila
kuathiri sheria za nchi, kila mtu ana uhuru wa kuwa na maoni, ingawa mwaka 2005
baada ya harakati mbaimbali zilizochukuliwa na wadau wa masuala ya uhuru wa habari, ilirekebishwa na ile sentensi ya: “bila
kuathiri sheria za nchi…” iliondolewa.
Kwa hali hiyo inamaana
kwamba pamoja na mabadiliko hayo kidogo katiba ya sasa ina sauti ya juu kuliko sheria
nyingine ndogo katika kulinda haki ya kila mtu kuwa na maoni au kukusanya,
kupokea na kusambaza taarifa, japokuwa bado ibara ya 30 inadhibiti uhuru huo.
Pamoja na hilo pia hadi
sasa ndani ya katiba hiyo bado kuna sheria zinazokwamisha uhuru wa vyombo vya
habari ikiwamo Sheria ya Magazeti ya 1976 ambayo, pamoja na mambo mengine,
inampa waziri mwenye dhamana ya masuala ya habari madaraka ya kufungia gazeti
lolote wakati wowote anapoona inafaa kufanya hivyo.
Sheria hiyo imekuwa
ikipigiwa kelele na wadau mbalimbali wa habari na asasi za kijamii kuanzia
mwaka 2001 ili ifanyiwe marekebisho na ile ya utangazaji ya mwaka 1993 ili ziweze kwendana
na wakati tuliopo.
Kutokana na kilio hicho
Serikali kwa kushirikiana na wadau waliweza kufanikisha kukamilika mchakato huo
mwaka 2003 ambao ulipewa jina la Sera ya Habari na Utangazaji 2003 na mwaka mwaka 2006 Serikali ilitaka kupeleka Muswada
wa Haki ya Kupata Habari kama ilivyoelekezwa katika sera mpya lakini
ukakataliwa na wadau wa tasnia hiyo baada ya kubaini makandokando yalikuwamo.
Hivyo wakaamua kukutana
na kuanza mchakato mwingine wa kuwashirikisha wananchi ili kupata maoni juu ya
sheria hiyo na baada ya mchakato huo wakaamua kuandika mapendekezo ya miswada miwili na
kuikabidhi serikalini.
Tangu mwaka 2009
mapendekezo ya wadau kuhusu muswada wa haki ya habari na huduma za vyombo vya
habari yalipowasilishwa Wizara ya Habari, Utangazaji na Michezo yamekwamia
pale, japo kila mara Serikali huahidi kuipeleka bungeni. Kupitishwa kwa muswada
huo kuwa sheria kungelimaanisha kufutwa kwa sheria mbaya kama ile ya magazeti
ya mwaka 1976 ambayo imekuwa ikitumika kufungia magazeti bila kufuata taratibu
za kimahakama au hata kutoa sababu za kuridhisha kitaaluma.
Ikumbukwe kuwa sheria
ya magazeti ya mwaka 1976 Namba. 1 ambayo inatakiwa kufutwa kutokana na kukinzana na misingi ya demokrasia ya uhuru wa vyombo vya habari pamoja na ya vyama
vingi.
Kinachojitokeza hapa ni
kwamba serikali inaonesha sura ya kupenda
kuendelea na sheria zake hizo za zamani
inazoamini hazitaweza kutoa uhuru zaidi kwa wananchi wake kutoa maoni, kujieleza, kujua na kupata kwa uhuru
zaidi kile kinachopitia katika vyombo vya habari.
Na ili hali hiyo iweze
kuondoka ni lazima kuundwa Katiba nyingine mpya ambayo itawapunguza makali
baadhi ya watendaji wa serikali waliopewa dhamana ya kusimiamia vyombo kuchukua
hatua kwa kukurupuka na kuvifungia vyombo hivyo bila kufanya uchunguzi wa kina.
Katiba na ifufuliwa sasa kwani wakati ni huu ili hapo badae pasitokee mungu watu wasiofuata sheria wala katiba mungu ibaliki tanzania mungu libaliki Jukwaa la Katiba Tanzania.
Comments
Post a Comment