JUKWAA LA KATIBA TANZANIA LAAZA KUFUFUA KATIBA MPYA

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Deus Kibamba, akizungum,za na wanahabari alipokuwa akisoma  taarifa ya maazimio ya mkutano Mkuu wa Kitaifa wa Katiba na Hatima ya Mchakato wa Katiba Mpya  Tanzania, uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Mazungumzo hayo yalifanyika Ofisi za Jukwaa hilo Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Jukwaa hilo Hebron Mwakagenda  
 Wanahabari wakichukua habari





                       MKWAMO WA KATIBA UANZE SASA

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Deus Kibamba, amemtaka Rais Dk. John Magufuli kufufua uanzihwaji wa katiba mpya uliokwama katika utawala uliopita, na kama hata fanya hivyo Jukwaa hilo litaaanzisha mikutano isiyokuwa na kikomo kwa ajili yakuitisha uundwaji wa katiba mpya.
Kibamba, akizungumza na wanahabari ofisini kwake wakati akisoma maazimio ya mkutano Mkuu wa Kitaifa wa Katiba ambao ulifanyika mwezi March 2, hadi 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam na kushirikisha wajumbe wapatao 150 wakiwakilisha vyama vya siasa, wabunge, Taasisi za Elimu ya Juu Mashirika ya Kimataifa, Wanahabari, Wahadhiri, Asasi za Kiraia na Kidini Pamoja na Makundi yanayotetea haki za Wanawake na Usawa wa Kijinsia.

Alibainisha kwamba katika mkutano huo kuliwasilishwa mada mbalimbali kuhusu Historia ya Katiba na uandishi wake Tanzania;. Matakwa ya Maslahi ya Zainzibar katika mchakato wa katiba mpya nchini na namna bora ya kuutatua ;, mchango wa vyombo vya habari katika mchakato wa katiba mpya nchini ;, wajibu wa asasi za Kiraia kwenye mchakato wa Katiba mpya ;, mapungufu katika sheria ya kura ya maoni kuhusu muda na matumizi yake pamoja na mchango wa wanawake katika kukwamua mchakato wa katiba mpya , aidha mkutano huo ulijadili na kuazimia juu ya mambo mbalimbali yanayohusu machakato na maudhui ya katiba mpya.

Maazimio ya Mkutano huo  ni kama ifuatoavyo;- Mkutano uliazimia  march 2 hadi 3 march 2017 uwe ni wa kwanza tu katika mfululizo wa mikutano kama huo itakayoendelea kufanyika hadi pale hatma ya mchakato wa katiba mpya nchini itakapojulikana.

2 Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli kwa nafasi yak aliyonayo kikatiba ndiye mtu pekee kwa sasa mwenye uwezo wa kuamua hatma aama kuokoa au kuangamizia mchakato wa katiba mpya nchini

3.Rais alitangazie Taifa juu ya tarehe rasmi ambapo mchakato wakatiba mpya utarejeshwa rasmi ikiwemo kuagiza kuchapishwa kwa tangazo lake katika gazeti maalum la Serikali (Governmrnt Gazette).4.Serikali itenge fedha kuanzia bajeti ya mwaka 2017 na 2018 katika fungu la Wizara ya Katiba na Sheria ili kuwezesha shughuli za awali katika kurejesha mchakato wa katiba mpya kuweza kuanza 5. Waziri wa katiba na Sheria Dk. Harrison Mwakyembe,aandae na kupeleke miswaada ya marekebisho katika sheria mbili zinazoongoza mchakato wa katiba mpya Tanzania, yaani sheria ya mabadiliko ya katiba No8 ya mwaka 2011 (Pamoja na marekebisho yake) na sheria ya kura ya maoni ya maka 2013 (kama ilivyorekebishwa). Hili lifanyike mapema kwenye mkutano wa saba wa bunge la kumi na moja unaoanza Apri 4 2017 kama sehemu ya mchango wake (waziri) katika kunasua mchakato wa katiba.

6. kuwepo na jopo maalum linaloshirikisha wataalam na wawakilishi wa makundi mbalimbali yanyofanyia kazi  masuala ya katiba na demokrasia likutane na Rais wa Tanzania ili kushauriana juu ya hatma ya mchakato wa katiba mpya na hatua bora ya kuuanzia kwa awamu hii ya pili ya mchakato wa katiba mpya na kwamba Jukata liratibu maandalizi ya mkutano huo na Rais.
7
. Jukata liratibu mchakato wa AZAKI kukutana na mamlaka mbalimbali ili kujenga hoja juu ya ukweli kwamba muda muafaka wakukamilisha mchakato wa katiba mpya ni sasa kabla ya kukaribia mno kwa uchaguzi mkuu wa 2020. Uzoefu wa JUKATA ni kwamba katiba mpya kokote duniani haiwezi kuandikwa wakati ambapo michakato ya kisiasa kama ya uchaguzi inakaribia kufanyika.
8
Mkutano Mkuu wa pili wa Kitaifa wa katiba uhusishe wajumbe zaidi kutoka uwakilishi mpana  wa makundi yote ya kijamii nchini ili kutoa fursa na wigo zaidi kwa madai mapya na muafaka wa kurejeshwa kwa mchakato wa katiba mpya nchini.9. Vyombo vya habari viwezeshwe kuendelea kutoa elimu juu ya historia, mchakato na maudhui ya katiba mpya kama sehemu ya kurejesha hamasa iliyojengeka wakati wa awamu ya kwanza ya mchakato wa katiba mpya na ambayo itahitajika sana katika ukamilishaji wa mchakato kwenye awamu ya pili.

10 Hitimisho;-Kutokana na Mkutano Mkuu wa kwanza wa Kitaifa wa katiba (MMKK11)na mikutano mingine iliyoandaliwa siku zahivi karibuni na kufanyika chini ya utaratibu wa makundi mbalimbali ikiwemo, mtandao wa wanawake na katiba Tanzania pamoja na Muungano wa Azaki Tanzania chini ya uratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu(THRDC) JUKATA likmezindua elimu ya uraia kupitia fursa mbalimbali kwa lengo la kujenga hoja juu ya haja ya kurejeshwa kwa mchakato wa katiba mpya hivi sasa na si baadaye. Aidha, JUKATA linatalaji kuwa maombi ya kukutana na Mheshimiwa Rais Dk Magufuli ambayo tayari yamefikishwa IKULU ya Magogoni Dar es Salaam yatapata majibu haraka kabra hajahamia Dodoma  ili kuwezesha JUKATA kutekeleza maazimio ya MMKK11.

Jukwaa hilo linamalizia kwa  kuwaomba Wananchi wote wa Tanzania  pamoja ana wanahabari kuungana nalo katika madai ya kurejeshwa kwa mchakato wa katiba mpya nchini mapema iwezekanavyo kwani kufanya hivyo ni kutekeleza masuala ya amani ya nchi pasiwepo na mapungufu ya aina yoyote yenye kutiliwa shaka pindi yanapofanyika maamuzi popote .


 kiBAMBA AKISISISTIZA JAMBA


Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.