Golf katika Klabu jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania Lugalo


Mcheza golf Mtoto Asnath Juma akiwa katika harakati za kupiga mpira katika mashindano yaliyohusisha vijana katika uwanja wa Klabu ya jeshi la Ulinzi la Wananchi ya Lugalo jijini Dar es Salaam (Picha na Luteni Selemani Semunyu).



Mashindano ya mwisho wa Mwezi ya  Mchezo wa Golf katika Klabu jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzani a  ya Lugalo yamefanyika huku Wachezaji wengi wakichezea viwango  vipya vya Uchezaji baada ya kufanya vizuri au vibaya katika mashindano ya Arusha Open na yale ya PWC yaliyofanyika Lugalo Jijini Dar Es Salaam.

Katika Division A mshindi ni Juma L ikuli aliyepiga mikwaju ya jumla 76 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 5 akifuatiwa na Saleh Mcharo  kwa count back  baada ys kupiga mikwaju ya jumla 77 huku kiwango cha uchezaji kikiwa ni Sita.

Katika Division B Raji Lavingia aliyeshinda baada ya kufungana (count back) baada ya kupiga mikwaju ya jumla 69 huku kiwango chake cha Uchezaji kikiwa ni 14 akifuatiwa na Shaizad
Bhanji aliyepiga mikwaju ya jumla 69 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 18.

Katika Kundi Cmcheza Golf Enock Magile  aliibuka na Ushindi baada kupiga mikwaju ya Jumla 72 akifuatia na Faidhal Mawji ambaye alishindaa baada ya kufungana (Count back ) baada ya kupiga Mikwaju ya Jumla 77 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 24.

Kundi la wazee Senior  katibu Mkuu wa Wizara ya ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa Mh Job Masima aliibuka na ushindi  baada ya kupiga mikwaju ya jumla 70 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 18 Akifuatiwa na Dk Edmund Mndolwa aliyepiga mikwaju ya jumla 78 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni Saba.

Kwa Upande wa Wanawake mshindi ni Sophia Mathias aliyepiga mikwaju ya Jumla 74 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 11 akifuatiwa na Vicky Elias aliyepiga mikwaju ya jumla 78 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni Nane.

Na kwa Upande wa Watoto George Kapinga aliibuka Mshindi baada ya kupiga Mikwaju ya Jumla 71 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 16 akifuatiwa na Mpiga Golf Zabron Khamis aliyepiga mikwaju ya Jumla 72 huku kiwango chake cha Uchezaji kikiwa ni 20.

 


Wacheza  golf Watoto wa Klabu ya Lugalo wakiwa katika picha ya pamoja  katika mashindano yaliyohusisha vijana wadogo katika uwanja wa Klabu ya jeshi la Ulinzi la Wananchi ya Lugalo jijini Dar es Salaam leo


Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.