Serikali yapongeza mpango wa Airtel FURSA • kikundi cha wanawake chapokea msaada wa shs milioni 10
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto) akikabidhi msaada wa mashine ya kutengeneza sabuni na vifungashio vyenye thamani ya zaidi ya milioni 10/- kupitia mpango wa Airtel FURSA ‘Tunakuwezesha’ kwa Mwenyekiti wa Kikundi cha Tupendane cha Tandika, Nasra Haji katika hafla iliyofanyika kituoni hapo Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Afisa Maendeleo ya Vijana wa Manispaa hiyo, Anna Marika.
Afisa Maendeleo ya Vijana wa Manispaa ya Temeke, Anna Marika (kushoto) akikabidhi kwa niaba ya Airtel msaada wa na vifungashio vya sabuni baada ya kampuni hiyo kukabidhi mashine ya kutengeneza sabuni vyenye thamani ya zaidi ya milioni 10/- kupitia mpango wa Airtel FURSA ‘Tunakuwezesha’ kwa Mwenyekiti wa Kikundi cha Tupendane cha Tandika, Nasra Haji katika hafla iliyofanyika kituoni hapo jijini Dar es Salaam jana. Wa (pili kushoto) ni Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi.
Serikali yapongeza mpango wa Airtel FURSA
·
kikundi cha wanawake chapokea msaada
wa shs milioni 10
Kufatia mchango wake katika maendeleo ya miradi ya vijana Serikali
imeupongeza mpango wa Airtel FURSA kwa kuwawezesha vijana nchi nzima kukuza
uchumi wao.
Hayo yamesemwa na Afisa maendeleo ya vijana wa wilaya ya
Temeke , Bi Anna Marica wakati Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA
ilipotoa msaada wenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa kikundi
kilichoundwa na wanawake 12 cha Tupendane kilichopo Temeke jijini Dar es salaam
Alisema” kupitia mradi wa Aritel FURSA, Airtel Tanzania
imekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia vijana nchini na kupongeza kikundi
cha Tupendane kwa kuwa moja kati ya vikundi vilivyofikiwa na Airtel FURSA
“Kikundi cha Tupendane kimeonyesha mfano mzuri hususani kwa
vijana wakike na napenda kuwahasa muongeze hari na kufanyakazi kwa bidii zaidi
ili kuongeza uzalishaji na kutengeneza ajira kwa vijana waishio jijini Dar es
salaam.” Alisema Marica
Msaada wa vifaa uliotolewa kwa kikundi hicho ni pamoja na mashine
mpya ya kutengenezea sabuni, vifungashio pamoja na kuboreshewa mazingira ya
ofisi ya kufanyia kazi.
Kwa upande wake Meneja huduma kwa jamii, Bi Hawa Bayumi
alisema“ tunatambua juhudi na ubunifu mkubwa unaofanywa na kikundi hiki
na tunaamini msaada huu utasaidia kuinua mapato yao kwa ujumla.
“Huu ni msimu wa pili wa mradi wetu wa Airtel FURSA ambapo
mpaka sasa tumeweza kuwafikia vijana wajasiriamali 20, makundi ya wajasiriamali
30 pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa zaidi ya vijana 3000 nchini. leo
tunajisikia furaha kukiwezesha kikundi hiki cha Tupendane kwani tunatambua kwa
kuwawezesha vijana hawa 12 tutaweza kuziwezesha familia zao na jamii kiuchumi
kwa namna moja au nyingine“ alisema Bayumi
Mwenyekiti wa kikundi cha Tupendane Nasa Hija Siri
aliwashukuru Airtel kwa kuwafikia vijana wengi na kutatua changamoto zao na
kuahidi kutumia msaada huo kuongeza uzalishaji
“ kupitia msaada huu tunauhakika wa kuongeza kiwango
cha uzalishaji wa bidhaa zetu kwani kwa sasa tunatengeneza lita 20 kwa siku, na
kwa msaada huu sasa tutazalisha hadi lita 100 kwa siku haya kwetu sisi ni
mafanikio makubwa na tunawashukuru sana Airtel”alisema Nasa
Kikundi cha tupendane kilianza biashara zake kwa kuuza
vitenge na kukopesa kwa wateja, biashara hii haikuwa ya mafanikio kwani wateja
walishindwa kulipa madeni yao kwa wakati ndipo walipoamua kuanzisha biashara ya
kutengeneza na kusambaza sabuni za maji na shampoo za nywele
Comments
Post a Comment