MISA TAN, MBATIA AKIWA VUNJO NA WALIMU


Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika(MISATAN) Bwana Andrew Marawiti  akizungumza jambo wakati akifungua kongamano na maafisa habari wa taasisi za serikali zilizofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi wetu
Maafisa habari mbalimbali kutoka wizara na mihimili tofauti ya nchi, jana walikutana katika hoteli ya JB Belmont hapa Dar es Salaam kujadili changamoto wanazo kumbana nazo wakati kwa kutoa taarifa kwa wananchi.
Kongamano hilo linafuatia matokeo ya utafiti wa upatikanaji taarifa kwenye taasisi za umma uliofanywa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) nakuzinduliwa rasmi siku ya tarehe 28 Septemba, ambayo pia ni Siku ya Kimataifa ya Haki ya Kupata Taarifa.

Miongoni mwa taasisi zilizoshiriki katika kongamano hilo ni Bunge, Mahakama, Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Nishati na Madini, Idara ya Habari Maelezo, Mamlaka ya Taifa ya Vitambulisho (NIDA) na Idara ya Taifa ya Takwimu. Wizara za Afya na Mambo ya Nje hazikuweza kuwakilishwa licha ya kupata mwaliko. 
 Mwanasheria kutoka Taasisi Kitaifa ya Msaada wa Kisheria (National Organization of Legal Assistance-nola)  Bwana James Malenga akisisitiza jambo alipokuwa anawasilisha mada yake kwenye kongamano hilo la maafisa habari wa taasisi za kiserikali lililoandaliwa na Misa-Tanzania.
Afisa Habari na Utafiti wa Misa-TanzaniaBwana Sengiyumva Gasirigwa akitoa ufafanuzi kwenye mada aliyokuwa anaiwasilisha kwenye kongamano la maafisa habari wa taasisi za kiserikali(hawapo picha)  
Mfanyakazi wa  Misa-TanzaniaBwana Idrisa Abdallah akizungumzia adha anazozipata anapokuwa anakwenda taasisi na idara mbalimbali za serikali kupeleka barua ama maombi ya taarifa.
Afisa habari wa Mahakama Bi. Mary C. Gwera akizungumza  jinsi ofisi yake ilivyopokea Tuzo ya Kufuli na ambavyo imekuwa chachu ya mabadiliko katika kutoa taarifa kwa umma.
Afisa Mwandamizi wa habari kutoka Idara ya Habari Maelezo Bwana Abraham Nyantori akielezea changamoto za utoaji taarifa katika taasisi na idara za serikali.



 Maafisa habari wakifuatilia kwa umakini mada ya Umuhimu wa Kutoa/Kupata Taarifa serikalini kutoka kwa mwanasheria wa kujitegemea Bwana James Marenga.
Kaimu Mkurugenzi wa Misa-Tanzania Bwana Andrew Marawiti  akitoa shukrani wa wageni waliofika kwenye kongamano hilo.

CWT WAADHIMISHA SIKU YA WALIMU DUNIANI

Mratibu wa Uhakiki wa Ubora wa Elimu kutoka Shirika la Kijamii la Masuala ya Elimu (Haki Elimu), Robert Mihayo akitoa mada kuhusu Ubora wa Elimu Tanzania wakati wa semina ya maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Semina hiyo iliandaliwa na TENMET kwa kushirikiana na Chama Cha Walimu Tanzania (CWT).
Mratibu wa Uhakiki wa Ubora wa Elimu kutoka Shirika la Kijamii la Masuala ya Elimu (Haki Elimu), Robert Mihayo akitoa mada kuhusu Ubora wa Elimu Tanzania wakati wa semina ya maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Semina hiyo iliandaliwa na TEN/MET kwa kushirikiana na Chama Cha Walimu Tanzania (CWT).
Ofisa Mradi wa TEN/MET, Alistidia Kamugisha (kulia), Meneja wa Fedha na Utawala (TEN/MET), Beatrice Malya (katikati) na Mratibu wa TEN/MET, Cathleene Sekwao. 
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
Neema Kitundu kutoka National Coordinator Fawetz.
Neema Kitundu kutoka National Coordinator Fawetz.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ukaguzi wa Shule Wizara ya Elimu ya Ufundi ya Ufundi, Dk. Edicome Cornel Shirima akitoa mada katika semina hiyo.
Mkurugenzi Mafunzo ya Ualimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bakari Issa akitoa mada katika semina hiyo.
Peter Mlimahadala kutoka Chama cha Walimu Tanzania akichangia mada katika semina hiyo. 
 Mratibu wa TEN/MET, Anthony Mwakibinga.

MBUNGE JAMES MBATIA ATEMBELEA MAKABURI YA WAZAZI WAKE NYUMBANI KWAO KILUA VUNJO

Marehemu ,Mwalimu Francis.W,Mbatia,Baba mzazi wa Mbunge wa Kuteuliwa James Mbatia.
Marehemu ,Philomena Francis Mbatia,Mama mzazi wa Mbunge wa Kuteuliwa James Mbatia.
Makaburi ya wazazi wa Mbunge wa kuteuliwa James Mbatia yaliyoko nyumbani kwao kata ya Vunjo Mangaribi-Kilua Vunjo wilaya ya Moshi vijijini.
Mh James Mbatia akiwa na viongozi wa Chama cha NCCR-Mageuzi mkoa wa Kilimanjaro wakati alipotembelea eneo hilo.
Mh James Mbatia akifanya sala mbele ya Makaburi ya Wazazi wake alipotembelea nyumbani kwao.
Mh James Mbatia akiwasilimulia viongozi alioambata nao mambo mbalimbali ambayo wazazi wake walipenda kumwelekeza yakiwemo maneno ambaye baadae aliamua yaandikwe juu ya makaburi hayo.
Mh Mbatia akiondoka katika eneo la Makaburi ya wazazi wake.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya kaskazini.

KAMPUNI YA COMSOFT YA UJERUMANI YA WAPIGA MSASA WAHANDISI NA WATAALAMU WA MASUALA YA USAFIRI WA ANGA BARANI AFRIKA.

  Kaimu Mkutugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya COMSOFT  Mr.Manfred Schmid (kushoto)wakimsikiliza kwa makini  Mkurugenzi wa Mradi wa Comsoft  Dr.Gunther Hellstrn ( kulia )wakati alipokuwa akitoa mada juu ya usimamizi wa mitambo ya ADS-B ambayo inatumika kwa ajilia ya usalama wa Anga  wakati semina iliyowahusisha wahandisi wa mamlaka ya usafiri wa Anga Barani Afrika iliofanyika leo ktika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ikiwa imeandaliwa na COMSOFT ya Ujeremani.
 Baadhi ya Wahandisi na wataalamu wa masuala ya usafiri wa anga kutoka barani Afrika wakimsikilza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya COMSOFT  Mr.Manfred Schmid (kushoto) wakati wa semina ya usimamizi wa mitambo ya ADS-B ambayo inatumika kwa ajilia ya usalama wa ndege ikiwa  kwenye anga husika.iliyofanyika katika hoteli ya serene leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya COMSOFT  Mr.Manfred Schmid  na Mkurugenzi wa Mradi wa Comsoft  Dr.Gunther Hellstrn ( kulia ) wakimsikilza kwa makini  mtaaramu wa kuongoza ndege kutoka Uganda (UGATCA) Magret Kagendo wakati alipokuwa akiuliza swali wakati wa semina iliyowashirikisha wahandisi na wataalamu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga barani Afrika iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wahandisi na wataalamu wa masuala ya usafiri wa anga kutoka barani Afrika wakimsikilza Mkurugenzi wa Mradi wa Comsoft  Dr.Gunther Hellstrn ( kulia ) juu ya masuala ya usimamizi wa usalama wa Anga  katika semina iliofanyika leo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
 Kaimu Mkutugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya COMSOFT  Mr.Manfred Schmid (kulia)wakimsikiliza kwa makini  Mkurugenzi wa Mradi wa Comsoft  Dr.Gunther Hellstrn ( kulia )wakati alipokuwa akiongelea masuala ya usimamizi wa usalama wa Anga  katika semina iliyowahusisha wahandisi wa mamlaka ya usafiri wa Anga Barani Afrika uliofanyika leo ktika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkutugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya COMSOFT  Mr.Manfred Schmid (kulia)wakiwa miongoni mwa washiriki wa semina ya  wahandisi na wataalamu wa uendeshaji wa mamlaka ya usafiri wa Anga barani Afrika iliyofanyika leo  katika hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam,Semina hiyo imeandaliwa na kampuni ya Comsoft ya Ujerumani ambao ni wataalamu wa mitambo inayotumika  kwa ajili ya usalama ndege wakati ikiwa anga husika.

Washiriki wa semina yamasuala ya mitambo ya ADS-B amabayo inatumika kwa ajili ya usalama wa Anga na Uangalizi wa Ndege inapotoka kwenye anga husika na kwenda naga nyingine iliyo wahusisha  Wahandisi na wataaramu wa masuala ya usafiri wa anga kutoka barani Afrika ,wakifuatilia moja ya mada zilizokuwa zikitolewa kwenye semina hiyo iliyoandaliwa na COMSOFT  jijini Dar es Salaam.

Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.