DAWASA NA HABITAT WALETA MAPINDUZI KATIKA ELIMU DAR
Meneja wa Mradi wa ujenzi wa mtambo wa nishati endelevu inayohifadhi mazingira (Biogas) kutoka UN-HABITAT Phillemon Mutashubirwa akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari walipotembelea mradi huo unaotekelezwa katika shule ya sekondari Manzese mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Meneja Uhusiano wa
Jamii Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA) Bi. Neli Msuya alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki walipotembelea mradi wa
ujenzi wa mtambo wa nishati endelevu inayohifadhi mazingira (Biogas) katika
shule ya sekondari Manzese iliyopo Mtaa wa Chakula bora kata ya Manzese Wilaya
Kinondoni jijini Dar es salaam. Mradi huo unatekelezwa shuleni hapo na DAWASA
kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa Makazi la Umoja wa Mataifa (UN-HABITAT).
Mratibu wa Mradi ujenzi
wa mtambo wa kuzalisha gesi ambayo ni
nishati endelevu inayohifadhi mazingira (Biogas) kutoka Taasisi ya Kuendeleza
Nishati Asilia na Uhifadhi wa Mazingira (TaTEDO) Shima Sago akieleza faida zitokanazo na
biogas kwa waandishi wa habari walipotembelea mradi huo unaotekelezwa katika
shule ya sekondari Manzese mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Mwalimu wa Taaluma wa shule ya sekondari Manzese Zubeda Kindamba akiushukuru uongozi wa DAWASA kwa kuendelea kuiunga mkono shule yao katika masuala mbalimbali ukiwemo Mradi wa ujenzi wa mtambo wa kuzalisha gesi asilia shuleni hapo.
Mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Manzese anayesoma masomo ya mchepuo wa sayansi Noela Shirima akielezea kwa waandishi wa habari namna watakavyonufaika mara utakapokamikika mradi wa gesi asilia itakayozalishwa na amesema kuwa kujengwa mradi wa gesi na maabara utawasaidia shuleni hapo kwa manufaa ya kupata elimu bora.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Chakula bora Kata ya Manzes Salehe Rashidi akielezea kwa waandishi wa habari walipotembelea shule ya sekondari Manzese mwishoni mwa wiki namna wananchi wake wanavyoshikiana na Uongozi wa shule hiyo katika kujali taaluma ya wanafunzi na afya zao kwa kufanya usafi katika maeneo yanayozunguka shule.
Mutashubirwa na Nelly, wakienda kukagua shimo linalochimbwa kuhusu kutebgebeza gesi
Mafundi wa Tatedo, wakiendelea na ujenzi
Darasa la Maabara
Majirani na shule hiyo wakitawanya mchanga uliotokana na uchumbwajai wa shimo lililosababisha kuzibwa kwa barabara ya mtaa huo
Comments
Post a Comment