PPF NA SHEREHE ZA MWAKA WAO DAR


 Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Dr Aggrey Mlimuka akizungumza na wafanyakazi wa mfuko wa pensheni wa PPF wakati wa sherehe ya Mwaka iliyofanyika katika Ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Jijini Dar Es Salaam Mwishoni mwa wiki.
 Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Dr Aggrey Mlimuka akiwapongeza Vijana wanaounda kundi la The Voice ambao ni wasanii wa fani ya Akapela mara baada ya Kutoa burudani katika sherehe ya Mwaka ya Mfuko wa Pensheni wa PPF iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Blue Pearl iliyopo Ubungo Jijini Dar Es Salaam.
Kundi la The Voice likitoa burudani katika sherehe ya Mwaka ya Mfuko wa Pensheni wa PPF iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Blue Pearl.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea katika Sherehe ya Mwaka ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF iliyofanyika mwishoni mwa Wiki katika Ukumbi wa Blue Pearl.
Afisa Mahusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Janeth Ezekiel akipokea cheti na zawadi kutoka Kwa Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Dr Aggrey Mlimuka mara baada ya kutangazwa kuwa mfanyakazi bora wa mwaka 2013 kutoka Idara ya Mahusiano na Masoko ya Mfuko wa Pensheni wa PPF katika sherehe ya mwaka ya PPF iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Blue Pearl, Jijini Dar Es Salaam
 Pichani Juu Ni baadhi ya wafanyakazi kutoka Idara Mbalimbali za Mfuko wa Pensheni wa PPF waliojipatia zawadi kwa kuwa wafanyakazi bora wa Mwaka 2013.
Wafanyakazi wa PPF wakifuatilia Burudani iliyokuwa ikitolewa na Kundi la The Voice katika Sherehe ya Mwaka ya PPF iliyofanyika mwishoni mwa Wiki katika Hotel ya Blue Pearl.
Mmoja wa wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF akimtunza Mmoja ya waimbaji wa kundi la the voice lililokuwa likitoa burudani wakati wa sherehe ya Mwaka ya Mfuko wa Pensheni wa PPF iliyofanyika Mwisho mwa Wiki katika hoteli ya Blue Pearl, Jijini Dar 
Wadau wakiserebuka Muziki mara baada ya wafanyakazi bora kupewa motisha na zawadi zao katika sherehe ya Mwaka ya PPF iliyofanyika Mwishoni mwa Wiki katika Hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Jijini Dar Es Salaam.

KINANA ASISITIZA WANANCHI BAGAMOYO KUJIUNGA NA MIFUKO YA AFYA YA JAMII

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwapungia mkono wakazi wa Bagamoyo wakati wakiwasili kwenye uwanja wa mkutano wa shule ya Msingi Jitegemee.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pongezi mshahiri maarufu wa CCM mkoa wa Pwani Ndugu Ali Pongwe baada ya kutoa ushairi mzuri kabla ya kuanza kwa mkutano.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Magomeni wilaya ya Bagamoyo ambapo aliwasisitiza kujiunga na mfuko wa afya ya jamii pamoja na wazazi kuwapeleka watoto shule pia aliwashauri wazazi kuchagua watu wenye shughuli zao kuingia kwenye kamati za shule kwani kutasaidia sana kupunguza michango isiyo ya lazima.
 Wananchi wa kata ya Magomeni wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Mwantumu Mahiza akihutubia wakazi wa kata ya Magomeni na kuwataka kuhakikisha watoto watakaochaguliwa kuingia sekondari wanaenda shule kwani kushindwa kufanya hivyo ni kurudisha nyuma maendeleo.Pia aliwataka wananchi wachunge afya zao kwani elimu ya maambukizi ya ukimwi inatolewa ya kutosha hivyo kila mtu anapaswa kuwa makini na afya yake.
 Sehemu ya watu waliohudhuria mkutano.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Magomeni ambapo alitoa sifa kwa Mkuu wa mkoa wa Pwani kwa utendaji wake wenye ufanisi mkubwa pia aliwaambia wananchi hao kuwa vyama vya siasa ndio vimeshafika muda wake kwani havina sera na vimeshindwa kuja na sera mbadala ya kuleta maendeleo ya kiuchumi nchini.
 Wananchi wakimsikiliza Nape Nnauye ambaye pia aliwataka watendaji wa Serikali kuwa karibu na wananchi kwani kutasaidia kufanikisha maendeleo na kuondoa sintofahamu za wananchi wanaotaka kujua taarifa za maendeleo ya miradi au maeneo husika.
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Dk.Shukuru Kawambwa akihutubia wakazi wa jimbo lake wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Jitegemee ambapo aliwaambia kero za michango midogo midogo zinaondolewa .
 Katibu wa CCM mkoa wa Pwani Joyce Masunga akihutubia wakazi wa kata ya Magomeni ambapo aliwaambia  wanawake kutokuwa nyuma katika kuomba nafasi za uongozi katika chaguzi zinazokuja.
 Mmoja wa wananchi waliofika kwenye mkutano akiuliza swali kwa Katibu Mkuu wa CCM wakati wa mkutano .

 Diwani wa kata ya Magomeni .Mwanaharusi Jarufu akijibu moja ya maswali yaliotoka kwa wananchi.
 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo akijibu maswali kutoka kwa wananchi
Sehemu ya wanachama wapya waliopokea kadi zao za uanachama leo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo zaidi ya wanachama 338 walijiunga na CCM.

UMOJA WA MATAIFA WATAKA CHANZO CHA SIASA KALI ZINAZOLETEA MIGOGORO KICHUNGUZWE

DSC_0007
Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh. Seif Rashid akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kuhudhuria maadhimisho hayo na kupokelewa na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Joseph Masasi (wa pili kulia), Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Bw. Dunford Makala (katikati) na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania , Bw. Ali Rajab (kulia) pamoja na viongozi wengine taasisi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinizim)

Na Mwandishi wetu

WAKATI Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon anahimiza serikali duniani kutafuta chanzo cha kukosekana kwa amani na kuongezeka kwa watu wenye misimamo mikali, wasemaji katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa amani Duniani wameitaka serikali ya Tanzania kutupia macho makali mauaji ya albino nchini.

Akimwakilisha Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika adhimisho lililofanyika viwanja vya Mnazi mmoja leo Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi mkazi wa UNDP nchini Alvaro Rodriguez, alisema ili kudumisha amani kuna mambo mengi yanatakiwa kufanyiwa kazi hasa kutambua chanzo cha migogoro inayosababisha msuguano mkubwa katika jamii na kukosekana kwa amani.

Alisema amani ina maana kubwa kwa jamii na ndio maana Umoja wa mataifa miaka 13 iliyopita iliamua kuadhimisha siku hiyo kwa lengo la kushawsihi makundi yanayosigana kupata nafasi ya kuzungumzia na kuona maana ya amani.

Alisema pamoja na kuwepo kwa hatua kubwa tangu kupitishwa kwa azimio la Umoja wa Mataifa la kuadhimisha amani, safari ya kufikia amani ni ndefu na ili kufanikiwa pande zote ni lazima kwenda hatua kwa hatua kwa kushirikiana.

Alisema mafanikio ambayo yamepatikana ni pamoja na UN kufanikiwa kufundisha kada ya habari juu ya uandishi katika mazingira tete na kusaidia majadiliano ya kitamaduni yanagusa masuala ya amani.
DSC_0031
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (katikati) akimtambulisha Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) mara baada ya kuwasili kwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania (THBUB), Bi. Mary Massay.

Aidha alisema kwamba wanafanyakazi na Wizara ya mambo ya ndani kuhakikisha kwamba wanastawisha mipango yote inayolenga kuzuia ghasia na kuboresha mipango inayoimarisha amani.

Akihutubia bada ya mashuhuda kuzungumzia hali ya tishio la amani nchini Tanzania hasa la kukosekana kwa amani miongoni mwa watu wenye ulemavu wa ngozi albino, Mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa aliipongeza serikali ya Tanzania kw ajuhudi zake za kuimarisha amani katika kanda ya maziwa makuu na kushiriki katika operesheni mbalimbali za Umoja wa Mataifa ziliziolenga kuleta hali bora zaidi ya maisha kwa watu wanaoishi katika hekaheka za kivita.

Akiwa na mwezi mmoja tangu awalisili nchini mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa nchini amesema kwamba anatarajia kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali na wananchi wa Tanzania kuhakikisha taifa la Tanzania linaendelea kuwa na amanai.

Wakati Mwakilishi huyo amesema kwamba watu wengi duniani wanawaonea gere wananchi wa Tanzania kwa amani wlaiyonayo, mwakilishi wa Under the Same Sun, Vicky Ntetema ametaka kupitiwa upya kwa sheria ya uchawi ya mwaka 1928 iliyofanyiwa mabadiliko mwaka 2002 ili kukabiliana na mauaji ya albino nchini ambayo kwa kiasi kikubwa yanachochewa na waganga wa kienyeji.
DSC_0039
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Seif Rashid meza kuu.

Alisema sheria hiyo ina mwanya mkubwa wa wauaji kucheza nayo na kusababisha sehemu kubwa ya kesi zilizopo kushindwa kuwatia hatiani wahusika.

Alisema wakati tukielekea katika uchaguzi mkuu mauaji ya albino na ukataji wa viungo umeongezeka.

Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi 25 za afrika zinazofanya ukatili dhidi ya walemavu wa ngozi, toka mwaka 2006 watu 74 wameuawa, 56 wamenusurika na 11 wameongezewa ulemavu huku makaburi 18 ya albino yakinajisiwa kwa kufukuliwa.

Watu wa kituo cha haki za binadamu wamesema pamoja na kuwepo na matukio 120 ya ukatili dhidi ya albino kesi 11 tu ndio zilizofikishwa mahakamani huku tano zikiwa zimekatiwa hukumu ambazo hazijaridhisha.
Vicky alisema katika matukio yote hayo chanzo ni ushirikina lakini kutokana na kukosekana zimeshindikana kuzimaliza zinavyotakiwa.
DSC_0082
Brass band ya jeshi la Magereza ikiongoza maandamano ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya amani wakiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho hayo jana.

Vicky aliitaka jamii kuwalinda albino kwani serikali pekee haiwezi kufanya kitu chochote huku akisema kwamba hesabu ya albino mmoja katika kila wananchi 1,400 haiwezi kulindwa kwa dhati na serikali kutokana na idadi ya polisi kutokua sawa na wananchi.

Aidha alishauri serikali kutoa msaada wa kisheria kwa waathirika kabla ya kuingia mahakamani ili waweze kusimulia vyema kadhia zao na pia wasiangushwe na wanasheria ambao wanatumia udhaifu wa kisheria kuwatoa watuhumiwa hatiani.

Pamoja na Vicky Ntetema kushawishi wananchi kulinda albino na kuwafichua wauaji Kaimu Mufti Sheikh Ismail Habibu Makusanya ameitaka serikali kuhakikisha kwamba kila mwananchi anapata utulivu wa kutosha kuendelea na shughuli zaka na kuhimiza mahakama kutenda haki.

Aliwakumbusha wananchi kama alivyosema Sydina Omar kwamba kila mmoja ataulizwa amefanya nini kukomesha madhila katika jamii wakati wa kiama na kusema serikali isipowajibika itasema nini na wananchi nao pia watajibu nini.
DSC_0100
Pichani ni baadhi wadau kutoka taasisi mbalimbali pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) wakiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja huku wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali za kuhamasisha amani nchini na kupinga mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) nchini wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani iliyofanyika jana jijini Dar.

Alisema amani hailetwi kama mvua , inatafutwa na kusema watu wasipotafuta amani na kuhakikisha amani inakuwapo itakuwa shida kubwa kwa taifa hili ambalo miaka yote limeogelea katika bahari ya amani.

Aliwasihi waumini wa Kiislamu na wananchi wengine kuhakukisha kwamba amani inakuwa ajenda ya kudumu kila wanapokutana pamoja.

Katika maadhimisha hayo ambapo wananchi walianza maandamano shule ya Uhuru Mchanganyiko hadi viwanja vya Mnazi mmoja, mgeni rasmi Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dk Seif Rashid alisema serikali imejipanga kuhakikisha inakomesha mauaji ya albino na kuwataka wananchi kuisaidia kwa kutokuwa waoga kutoa ushahidi na pia kuwaripoti watuhumiwa.

Alisema kauli mbiu ya mwaka huu ya haki ya amani kwa watu wote, komesha mauaji ya albino inahamasiaha umma wa Tanzania kulaani,kukemea na kukomesha mauaji kwani yanakwenda kinyume na katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 14 ambayo inaeleza kwamba kila mtu ana haki ya kupata hifadhi katika jamii.

Aidha waziri alitaka kutekelezwa kwa agizo lake kuhusu tiba mbadala na za asili na kusema serikali itaendelea kulinda amani na kutoa ulinzi kwa wathirika.
DSC_0108
Meza kuu ikipoeka maandamano ya siku ya kimataifa ya amani kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
DSC_0248
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Joseph Masasi akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi Mh. Seif Rashid (wa pili kulia). Kutoka kushoto ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Bw. Dunford Makala, Balozi wa Uturuki nchini, Mh. Ali Davutoglu.
DSC_0593
Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh. Seif Rashid, akisoma hotuba kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
DSC_0415
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-Moon kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani duniani.
DSC_0418
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akipongezwa na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mh. Ali Davutoglu baada ya kusoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
DSC_0279
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema akisoma risala yake kwa mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
DSC_0284
Kaimu Mufti Sheikh Ismail Habibu Makusanya, akizungumza kwenye maadhimisho hayo ambapo alilaani vikali mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinizim) na kusema kuwa watu wote wanaoshiriki katika mauaji hayo kamwe hawatoiona Pepo ya Mwenyezi Mungu.
DSC_0384
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mh. Ali Davutoglu akisoma ujumbe kwa niaba wa umoja wa mabalozi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani duniani.
DSC_0300
Baadhi ya wadau kutoka taasisi na asasi mbalimbali nchini walioshiriki kwenye maadhimisho hayo.
DSC_0420
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania (THBUB),  Mary Massay akitoa nasaha kutoka kwa Tume hiyo, ambapo alitoa rai kwa mtu yeyote yule ambaye ana malalamiko au matatizo katika Haki za Binadamu anakaribishwa kwenye tume hiyo kwa ajili kupata msaada wa kisheria.
DSC_0519
Shuhuda aliyenusurika kwenye mauaji ya Albino ambaye amekatwa mikono yote miwili, Mariam Stanford akitoa ushuhuda wake na killio chake mbele ya meza na wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mnazi mmoja.
DSC_0534
Mke wa Balozi wa Uturuki nchini Yesim Davutoglu, akilia kwa uchungu baada ya kusikia shuhuda kutoka kwa mhanga wa mauaji ya Albino aliyekatwa mikono yote miwili, Mariam Stanford (hayupo pichani) ambaye hadi sasa anapewa matunzo na Shirika la Under The Same Sun.
DSC_0540
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema akimfariji mke wa Balozi wa Uturuki nchini Yesim Davutoglu, wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar.

MKUU WA WILAYA YA MAKETE AFANYA KIKAO CHA MAENDELEO NA WANAMAKETE WAISHIO JIJINI DAR

 Mkuu wa wilaya ya Makete  Josephine Matiro akizungumza katika kikao hicho.

Wananchi waliozaliwa wilayani Makete mkoani Njombe ambao wanaishi nje ya wilaya hiyo, wameshauriwa kuipenda wilaya yao kwa kuja kuwekeza pamoja na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo ndani ya wilaya hiyo

Rai hiyo imetolewa hii leo na Mkuu wa wilaya ya Makete  Josephine Matiro katika kikao baina yake na wananchi wa Makete waishio jijini Dar es Salaam kilichofanyika jijini humo
Katika kikao hicho mkuu wa wilaya amewashirikisha mambo mengi ya kimaendeleo katika wilaya ya Makete ikiwemo uwepo wa shule ya sekondari ya wasichana ya Makete Girls secondary ambayo pamoja na kuanza kufanya kazi bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali

Mh. Matiro amezitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ukosefu wa bweni na kuwa wanafunzi wanalala kwenye vyumba vilivyojengwa kwa ajili ya madarasa, bwalo, jiko pamoja na maabara ambavyo vinatakiwa viwepo

Amewaomba wananchi hao kuunga mkono kwa jinsi Mungu alivyowajalia na kwamba yeyote atakayejisikia kuchangia anaombwa kufanya hivyo kwani kila mmoja kwa nafasi yake ana mchango katika shule hiyo ili iondokane na changamoto hizo
"Ndugu zangu wilaya yetu inawatambua sana. tunaomba na tunahitaji sana ushirikiano wenu katika maendeleo ya makete, tukishirikiana kwa pamoja kwa kadri Mungu alivyotujalia kwa hakika shule hii itaimarika sana" amesema Matiro

Kwa upande wao washiriki wameoneshwa kufurahishwa na maendeleo ya kasi katika wilaya ya makete huku wakiipogeza serikali kwa juhudi zake za maendeleo hasa katika elimu, barabara, umeme pamoja na mambo mengine huku wakisema wataunga mkono maendeleo ya wilaya yao kwa kadri ya uwezo wao
Pia wameonesha kufurahishwa na Matiro kuwatafuta na kuzungumza nao kwani wamesema amekuwa mkuu wa wilaya wa kwanza kuzungumza nao toka wilaya hiyo imeanzishwa na kumtaka kuwa na moyo wa kuipenda wilaya ya Makete kama mkuu wa wilaya
 Wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya.

Baada ya kushirikishwa hivyo wameahidi kushirikiana na mkuu huyo wa wilaya kutatua changamoto hizo


RASIMU YA KATIBA MPYA ILIYOPENDEKEZWA KUWASILISHWA BUNGENI SEPTEMBA 24 MWAKA HUU

Na Benedict Liwenga na Magreth Kinabo.

RASIMU ya Katiba  Mpya  iliyopendekezwa inatarajiwa  kuwasilishwa  katika Bunge Maalum la Katiba Septemba 24, mwaka huu.
Mabadiliko hayo yametangazwa leo jioni na Katibu wa Bunge Maalum la Katiba, Yahya Khamis Hamad wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Aidha Katibu huyo amesema uamuzi wa mabadiliko hayo, umetokana na kufanyika kikao baina ya Kamati ya Uongozi wa Bunge hilo na Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi. 
Hata hivyo Katibu huyo amesema kuwa kazi ya uandishi wa Rasimu hiyo imeshakamilika na kazi iliyobakia ni kuipitia kwa makini, hali iliyosababisha mabadiliko ya uwasilishaji wa Rasimu hiyo katika Bunge hilo, uliopangwa kufanyika hapo kesho Septemba 22, mwaka huu.
“Uwasilishwaji wa Rasimu ya Katiba inayopendekezwa sasa utafanywa siku ya Septemba 24, mwaka huu, ” alisema Katibu wa Bunge hilo.
“Kamati ya uongozi imeona kuwa ni busara na kupewa siku mbili kwa ajili ya kuipitia upya ile kazi ambayo wameifanya ili kufikia tarehe 24 kutoa kitu makini, napenda niwahakikishie wananchi kuwa kitu kizuri kinakuja.
Aliongeza kuwa Kamati ya Uongozi ya Bunge hilo, inatarajia kukabidhiwa Rasimu ya Katiba Mpya iliyopendekezwa tarehe 23 Septemba, mwaka huu kutoka kwa Kamati ya Uandishi wa Bunge hilo.
Aidha, Katibu huyo ameeleza sababu ya uairishwaji wa uwasilishwaji wa Rasimu hiyo Bungeni hapo kutokana na ugumu, umakini na uzito wa kazi yenyewe.
“Tulikuwa tumepanga hapo tokea awali kufanya kikao na Kamati ya Uongozi asubuhi tukafanya mchana na hata jioni kila wakati Kamati ya Uandishi ikawa bado haijamaliza hiyo kazi na tulivyofanya kikao cha Kamati ya Uongozi hii jioni tukamuita Mwenyekiti wa Kamati ya uandishi akaonyesha kwamba hiyo kazi walikuwa wakiifanya usiku na mchana na hadi sasa wamesema wamemaliza kuandika.
“Lakini kutokana na namna walivyokuwa wakiifanya hiyo kazi kwa uharaka na ingawa walikuwa wakiifanya kwa umakini lakini wanahitaji muda wa kuanza kuipitia kwa makini zaidi kuanzia mwanzo mpaka mwisho hivyo wakaomba wapewe muda wa siku mbili ya kesho na keshokutwa ili kuweza kuipitia kazi hiyo kwa umakini,”alisema.
Katibu wa Bunge hilo, aliongeza kwamba mabadiliko hayo hayataweza kuathiri upigaji kura uliopangwa kufanyika Septemba  29  hadi 2 Oktoba mwaka huu.
“Tumeacha  siku ya Septemba  29, mwaka huu  ili iwe siku ya kuanza kupiga kura na tumalize 2 Oktoba, mwaka huu ili tuhakikishe kwamba Oktoba  4 , mwaka tumemaliza hili zoezi,” alisisitiza.
Aidha Katibu huyo alifafanua kuwa ratiba kuhusiana na masuala hayo  ataitoa 

SIMBA NA WAGOSI WA KAYA TAIFA

Beki wa Simba, Mohamed Hussein (kulia) akichuana na Seleman Rajab. Timu hizo zilitoka sare ya 2-2.
Emmanuel Okwi akiwania mpira na beki wa Coast Union.
 Umati wa mashabiki waliofika uwanja wa Taifa.
 Mshambuliaji wa Simba, Ramadhan Singano 'Messi' akimiliki mpira huku akizongwa na beki wa Coast Union, Abdallah Mfuko.
Mshambuliaji wa Simba, Haruna Chanongo akiruka daruga la beki wa Coast Union. 
 Hamis Tambwe akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Coast Union.
Hatari katika lango la Coast Union.
Emmanuel Okwi akimtoka beki wa Coast Union.
 Kikosi cha Simba.
 Kikosi cha Coast Union.
 Golikipa wa Coast Union ya Tanga, Shaban Kado akiokoa moja ya hatari langoni mwake.

Wachezaji wa Coast Union wakitoka mapumziko.

Wachezaji wa Simba wakitoka mapumziko.
 Benchi la ufundi la Coast Union.
 Manahodha wa Simba na Coast Union wakiwa katika picha ya pamoja.
Benchi la ufundi la Simba likiongozwa na Patrick Phil.
Kikundi cha New Mapambano kikitumbuiza wakati Simba ikipambana na Coast Union.
 Mashabiki wa Simba wakiwa na uzi wa Simba.
 Mashabiki wa Simba wakiishangilia timu yao.
 Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la kwanza la timu hiyo kabla Coast Union kusawazisha.
Mshambuliaji wa Simba, Hamis Tambwe akiifungia timu yake bao la pili wakati timu hiyo ilipopambana na Coast Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 2-2.

Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.